DUNIA haiishi vituko, nakuletea hii kutoka Marekani ambapo mwalimu anayefundisha watoto wadogo katika shule moja iliyopo New Jersey amezua gumzo mitandaoni baada ya wazazi wa watoto anaowafundisha kuja juu kutokana na maumbile makubwa aliyonayo mwalimu huyo.
Mwalimu huyo wa masomo ya sanaa @toyboxdolls anawafundisha wanafunzi chini cha miaka 5, wazazi wamemshambulia mitandaoni kwa namna anavyovaa mavazi yasiyo na heshima lakini kubwa zaidi likiwa ni juu ya maumbile yake makubwa aliyonayo.
Baadhi ya wazazi wamesikika wakisema, tatizo siyo nguo anazo vaa mwalimu huyo, bali tatizo ni maumbile yake. Pia wazazi wanaamini kitendo cha watoto wao kuona umbo kama hilo itapelekea tabia mbaya kwa watoto hapo baadaye.
Unafikiri wazazi wapo sahihi , au ni ukorofi tu?
Social Plugin