Kakakuona
Mnyama aina ya Kakakuona ambaye ni nadra sana kuonekana hadharani amekutwa katika eneo la Mpiji lililopo Maili Moja wilayani Kibaha mkoani Pwani, nyumbani kwa Mzee Mkwenya, huku wananchi wakionekana kumshangaa kiumbe huyo wa ajabu.
Imezoeleka kuwa tangu enzi za mababu pindi anapoonekana mnyama huyo basi wakazi wa maeneo husika huweka vitu mbalimbali ikiwemo nafaka kama ishara ya kupata ubashiri wa jambo litakalojitokeza kwa siku za mbeleni.
Mara baada ya mnyama huyo kuonekana, wazee wa kimila walimfanyia mambo ya kimila, walimwekea mpunga, mahindi na baadhi ya silaha kwa namna ambavyo wao waliona itafaa.
Chanzo - EATV