Kijana wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) jijini Arusha, Nathan Kimaro amemzawadia nakala ya kitabu cha aliyekuwa Rais wa awamu ya pili Mhe.Ali Hassan Mwinyi (MZEE RUKHSA), Msomi na Mwanajumui wa Afrika (Pan-Africanist) Profesa Patrick Lumumba hapo jana jijini humo.
Prof Lumumba alikuwa mgeni mwalikwa kwenye mkutano wa Kimataifa ulioandaliwa na Taasisi ya WAJIBU , uliofanyika kwa siku mbili (Novemba 18-19,2021) jijini Arusha uliohusu masuala ya Uwazi, na Uwajibikaji kwa mwaka 2021 (International Transparency and Accountability Conference 2021 (ITAC 2021).
Social Plugin