Kikosi cha Cameroon baada ya kuinyuka Ivoery Coast kwa kuichapa bao 1-0
Cameroon imefanikiwa kuwa miongoni wa mataifa 10 ambayo yamefuzu katika kinyang'anyiro cha kucheza fainali za kombe la Dunia za mwaka 2022 zitakazopigwa nchini Qatar baada ya kuinyuka Ivory Coast kwa bao 1-0
Bao pekee na la ushindi la Cameroon lilifungwa na Karl Toko Ekambi ambaye anakipiga na Klabu ya Lyon ya Ufaransa na sasa Indomitable Lion wanafuzu kwa mara ya 7 katika hatua hiyo ikiwa ni rekodi kwa bara Afrika.
Mataifa yaliyofuzu hatua ya mtoano ni Senegal,Morocco,Algeria ,Nigeria, Misri,Cameroon,Mali,Ghana na DR Congo ambazo zitapagiwa droo mnamo Mwezi machi mwaka 2022.
Mataifa 10 ya Ulaya yaliyoongoza makundi ya kufuzu kombe la Dunia mwaka 2022 na kukata tiketi ya kushiriki moja kwa moja;
🇷🇸Serbia
🇪🇸Spain
🇨🇭Switzerland
🇫🇷France
🇧🇪Belgium
🇩🇰Denmark
🇳🇱Netherlands
🇭🇷Croatia
🏴England
🇩🇪Germany