WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI SEKTA YA MISITU NA CHAPA YA MKOA WA IRINGA



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefungua  Kongamano kubwa la uwekezaji katika sekta ya misitu huku akitoa pongezi kwa mkoa huo na kueleza msimamo wa Serikali ya awamu ya sita katika kuchochea uwekezaji nchini.

 Pia Waziri Mkuu aliagiza makampuni yenye kuchakata mazao ya misitu kuhakikisha yanatengeneza bidhaa bora na kutosafirisha bidhaa ghafi.

Kabla ya kufungua kongamano hilo alizindua chapa ya Iringa woodland ikiwa ni lengo la mkoa wa Iringa kuchagiza ukuaji wa utengenezaji wa bidhaa za mbao, kuutangaza mkoa na pia utalii.

Waziri Mkuu aliuelezea mkoa wa Iringa kama eneo bora la uwekezaji likiwa na muunganiko mzuri wa barabara na muda mfupi ujao kwa ndege baada ya kukamilika kwa uwanja wa ndege wa Iringa.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendega alisema mkoa wake uko tayari kusaidia wafanya biashara kufanya biashara kwa urahisi kwa kuweka mazingira wezeshi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa Gofin Ventures Imani Kajula ambao ni waandaaji wa kongamano hilo na mkakati wa kujenga chapa ya Iringa woodland alisema " hii ni fursa pana kwa mkoa wa Iringa kufaidika na sekta ya utalii, misitu na pia kuutangaza mkoa wa Iringa ndani na nje ya Tanzania" pia kutoa ajira kwa vijana ambao watatumia chapa ya Iringa woodland kutengeneza bidhaa mbali mbali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post