Watu wasiojulikana wamedaiwa kumbaka mwanamke mmoja hadi kufariki dunia na mwili wake kukutwa kwenye shimo la taka (dampo) katika Mtaa wa Mtwivila C uliopo Manispaa ya Iringa.
Mwili wa mwanamke huyo aliyetambuliwa kwa jina la Rehema Lukosi (57) mfanyabiashara maarufu wa mboga mboga na bagia kwenye mtaa huo umekutwa eneo la tukio na wapita njia waliokuwa wanapita asubuhi.
Chanzo - Mwananchi
Social Plugin