MSHINDI wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Malala Yousafzai raia wa Pakistan amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Asser Malik katika jiji la Birmingham nchini Uingereza.
Maisha ya binti huyo yaliwagusa wengi baada ya kushambuliwa na wanamgambo wa Taliban alipokuwa na umri wa miaka 15 kwa kupigwa risasi ya kichwa alipokuwa akitoka shuleni huko kwao Pakistan mwaka 2012.
Malala alipona na kuhamia Uingereza, baadaye alipata nafasi ya kusoma katika Chuo Kikuu cha Oxford na mwaka 2017 akaweka rekodi ya kuwa mtu mdogo zaidi kupewa tuzo ya Nobel kwa mchango wake wa kutetea haki za wasichana kupata elimu. Kwasasa Malala ana umri wa miaka 24.
Asser Malik ni kiongozi maafuru wa Soka la Cricket nchini Pakistan ambapo anahudumu kama Meneja Mkuu katika Bodi ya Cricket Pakistan. Malik ni msomi wa shahada ya uchumi na Sayansi ya Siasa kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi ya Uongozi cha Lahore. Amefanya kazi na makampuni makubwa duniani kama Coca Cola na FrieslandCampina.
Malala na Asser wamekuwa kwenye uhusiano wa siri tangu mwaka 2019, mpaka jana Jumanne walipoamua kufunga ndoa ya Kiislam na kufanya sherehe yao nchini Uingreza.
Social Plugin