Mshukiwa Yvonne Wanjiru anasemekana kumvamia kwa kisu mke mwenza Bernice Wangeci ambaye alikuwa ameenda nyumbani kwa mumewe bila ya matarajio yake siku ya Jumanne, Novemba 2,2021.
Akidhibitisha kisa hicho, OCPD wa Subukia Patricia Nacio alisema Yvonne mwenye umri wa miaka 25 aliletewe mke mwenza Bernice na mumewe akiwa nyumbani.
Aidha, Nacio aliwaonya wanandoa dhidi ya kujichukulia sheria mikononi na kusababisha vifo vya kiholela.
Baada ya kutelekeza kitendo hicho, Nacio alisema mshukiwa alitoroka na kwa sasa anasakwa na maafisa wa polisi.
Mwathiriwa Bernice alikimbizwa katika hospitali ya Subukia lakini alikata roho kabla ya kuhudumiwa na madaktari.
Chanzo - Tuko News
Social Plugin