Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KIJANA AMUUA MAMA YAKE KWA TEKE AKIINGILIA UGOMVI AKIPIGANA NA KAKA ZAKE



Polisi mjini Kakamega nchini Kenya wamemkamata mwanaume mwenye umri wa miaka 35 kwa madai ya kumuua mamaake kwa kumpiga teke alipokuwa akijaribu kuwatenganisha akipigana na kaka zake wawili.

Kulingana na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Makomere Shikokongo alimpiga teke mamaake mwenye umri wa miaka 60 alipokuwa akiwatenganisha wakati wakizozana kuhusu masuala ambayo bado hayajajulikana 

Mtuhumiwa na ndugu zake wawili; John Omoro (25) na Joseph Amakobe (40) walikuwa wakizozana kuhusu masuala ambayo bado hayajajulikana hadi sasa kwa mujibu wa Citizen Digital. 

DCI ilibaini kuwa babaake ndugu hao Paul Shikokongo mwenye umri wa miaka 63 hakuwapo wakati wa kisa hicho, na ndiposa mama yao akaingilia kati na kuwatawanya.

 "Ijumaa usiku, mwanamke mwenye umri wa miaka 60 ambaye alilalamika kuumwa na mwili kutokana na shambulio hilo, alifariki dunia akiwa nyumbani kwake kwa vile hakuwa amepelekwa hospitalini kwa matibabu," DCI ilisema.

Kwa sasa Shikokongo anazuiliwa na polisi akisubiri kufunguliwa mashtaka.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com