Afisa Sera na Majadiliano wa TFCG Elida Fundi akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kamati Mpya ya Maliasili Agatha Gambe akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa Mtandao wa Wazalishaji Mkaa kwa njia Endelevu wa Wilaya ya Kilosa Kulangwa Ganda akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Enyasi Simon akizungumza kwenye mkutano huo.
Philemoni Robert akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wajumbe wa Kamati ya Maliasili wakiwa kwenye mkutano huo.
Picha ya pamoja.
MRADI wa Kuhifadhi Misitu kupita biashara Endelevu ya mazao ya misitu unaotekelezwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa jamii wa usimamizi wa Misitu (MJUMITA)kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswis (SDC) umewanufaisha Wananchi wa Kijiji cha Ihombwe kilichopo Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mikumi mkoani Morogoro kwa kukamilisha
miradi kadhaa ya maendeleo.
Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Vashty Chimile wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari na maafisa wa Mradi ambao wapo katika ziara ya kujifunza kuhusu utekelezaji wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu mkoani hapa.
Chimile alielezea mafanikio yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa shighuli za usimamizi wa nMisitu kijiji hapo ikiwemo utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kutokana na fedha zinazotokana na tozo za uzalishaji wa mazao ya Misitu kwa njia Endelevu ambao o hapo awali kabla ya mradi huo walikuwa hawazipati.
Alisema mradi huo katika kijiji hicho ulianza Mwaka 2012 kwa kuanza kutengeneza mipango ya matumizi bora ya ardhi na mipango ya usimamizi wa Misitu na kupatiwa mafunzo mbalimbali. Kijiji kiliaanza kuvuna na kuingiza kipato mwaka Julai 2014 ambapo mapato ya kwanza yalikuwa ni zaidi ya Sh.33.5 Milioni na hadi kufikia mwaka 2021 walikuwa wamekusanya zaidi ya Sh.259.Milioni.
Alisema mpaka sasa fedha zilizotumika ni zaidi ya Sh.189 Milioni na benki zipo Sh. 70 milioni mbazo zimefanyiwa mpango wa matumizi mpaka mwaka wa fedha wa 2021/2022.
Alitaja matumizi ya fedha hizo kuwa wameweza kuchonga barabara ya kilomita tisa, ujenzi wa madarasa matatu ya shule ya Msingi kwa Sh.45 milioni, uchimbaji wa kisima cha maji cha mita 121 kwenda chini na kujenga nyumba ya mganga wa zahanati ya kijiji, kujenga vyoo katika nyumba za watumishi wa Serikali waliopo kijijini hapo, kuweka umeme katika ofisi zote za taasisi za Serikali, kununua baadhi ya vifaa katika wodi ya wazazi wa zahanati hiyo na mwaka 2014/ 2015 walifanikiwa kuwalipia bima ya afya wananchi wote wa kijiji hicho.
Mkazi wa Kijiji hicho Philemon Robert alisema kabla ya kuanza mradi huo kulikuwa na uharibifu mkubwa wa misitu ya ukataji wa miti hovyo kwa ajili ya uchomaji mkaa na mbao laking baada ya kuanza mpango huu wa Usimamizi shirikishi wa Misitu na biashara Endelevu ya mazao ya Misitu wamepata mafanikio makubwa ya kukusanya mapato mengi kutokana na kuuza mkaa endelevu na mbao.
Afisa Uhusiano wa TFCG Bi, Bettie Luwuge aliwaomba wananchi wa kijiji hicho kuwapa ushirikiano wajumbe wa kamati mpya ya maliasili iliyochaguliwa hivi karibuni ili waweze kufanya kazi zao kwa weledi zaidi.
Afisa Sera na Majadiliano wa MJUMITA Elida Fundi alisema usimamizi shirikishi wa misitu ya jamii ni dhana ambayo ikitekelezwa vizuri zaidi itasaidia wananchi kupata maendeleo yao na kuokoa misitu ambayo inaendelea kupotea kwa kiwango kikubwa kwenye ardhi ya vijiji isiyokuwa chini ya usimamizi maalumu.
Katibu wa Mtandao wa Wazalishaji Mkaa kwa njia Endelevu wa Wilaya ya Kilosa Kulangwa Ganda alisema mafunzo mbalimbali waliyopewa na mashirika haya yamesaidia sana kutekeleza shuhguli za Usimamizi wa Misitu ya jamii vizuri. Mafunzo haya yamewasaidia kuelewa wajibu wao wa utumzaji wa Misitu badala ya kuwachia serikali hasa dhana iliyojengeka kwa wananchi kuwa anayepaswa kuilinda ni Serikali na kuwa sasa mapato yameanza kuonekana.
Social Plugin