Nakuletea hii kutoka pande za Joe Biden, Marekani ambapo kichanga aliyezaliwa katika wiki ya 21 huku akiwa na uzito wa 420g, amevunja rekodi ya dunia ya kuwa kichanga aliyezaliwa kabla ya muda wake lakini akapata bahati ya kuendelea kuishi.
Madaktari wameeleza kuwa ni nadra mno kwa kichanga anayezaliwa katika wiki ya 21 kuendelea kuishi, mama wa kichanga hicho alikimbizwa hospitali Julai 4, 2020 ambapo alijifungua watoto wawili Curtis na C’Asya isivyo bahati dakika chache baada ya kujifungua, C’Asya alifariki dunia huku akimuacha Curtis ambaye alikuwa kwenye hali mbaya.
Curtis aliwekwa kwenye uangalizi mkubwa wa madaktari bingwa huku akiwa kwenye mashine maalumu ya ‘Ventilator’ ambapo alidumu kwa siku 275 hospitalini na baadaye kuruhusiwa. Guinness World Record imethibitisha kuwa mtoto huyo kwa sasa ana miezi 16 na afya yake ni njema, na hivyo kuweka rekodi ya dunia ya kuwa kichanga aliyezaliwa kabla ya muda na kupata nafasi ya kuendelea kuishi.
Social Plugin