Ni ndege pekee nayaejulikana kuwa na maumbile ya kitu kinachofanana na pembe katika kichwa chake .Kwa jina la kiingereza huitwa na Horned screamer.
Katika kipindi cha maisha yao, ndege hao hukua miiba mirefu yenye rangi nyeupe katikati ya paji la uso wao.
Ndege wengine wana pembe zinazokaribia inchi sita kwa urefu. Kulingana na makal iliyochapishwa na National Geographic hakuna ndege wengine duniani walio na kitu kama hicho.
Tofauti na kondoo dume na vifaru, pembe ya ndege huyo haionekani kuwa silaha, kwa sababu inashikamana kwa urahisi kwenye fuvu la kichwa na inajulikana kukatika mara inapokua ndefu sana.
Baada ya muda, pembe zilizovunjika hata hukua tena. Hii inasababisha wanasayansi kuamini kwamba pembe hizi hutumikia kusudi la mapambo badala ya kufanya kazi.
Wakati pembe hizi hazina madhara, ndege hawa ni hatari. Kila ndege ana jozi ya mfupa ulioinuliwa juu ya mbawa zake. Hizi hutumiwa kutetea eneo na vita kati yao kupigania wapenzi. Baada ya makabiliano mabaya sana, wanasayansi wamepata hata vipande vya chembechembe vimevunjwa na kuwekwa kwenye kifua cha ndege wengine.
Kando na pembe zao za ajabu, ndege hawa pia wana maumbile ya kuvutia chini ya uso.
Ndani ya mifupa na ngozi zao kuna tani za vifuko vidogo vya hewa vinavyopunguza uzito wa ndege hao wakubwa, jambo linalofikiriwa kuwasaidia kuruka umbali mrefu bila kutumia nguvu ya misuli.
Mifuko hii ya hewa wakati mwingine hujifunga wakati wanapopaa, na kusababisha kelele kubwa ya mlio.
Kama jina lake linavyodokeza, ndege huyu pia anajulikana kwa milio mikubwa . Sauti hiyo inafafanuliwa kuwa inasikika kama, "mo-coo-ca," inayowafanya baadhi ya watu wa kiasili kuwaita ndege hao "mahooka."
Makaazi na Lishe
Ndege hawa wanaweza kupatikana kutoka Colombia na Ecuador hadi kusini-kati mwa Brazili. Kama binamu zao wa karibu, bata-bukini, ndege hao hupendelea makazi yenye unyevunyevu, kama vile rasi za maji baridi, savanna zenye mvua nyingi za kitropiki, na maziwa.
Kama wanyama walao majani, ndege hawa wenye pembe hutumia muda mwingi wa siku kula nyasi zinazopatikana ndani na karibu na maji. Ndege hao pia wameonekana wakitafuna majani, mashina, maua na pia wakichimba kwenye matope.
Ingawa inaweza kuchukua mapigano ili kupata mwenzi, ushirikiano wa ndege hawa unaweza kudumu maisha yote. Mwanaume na jike huwa pamoja kwa mwaka mzima pamoja, wakitunzana kila mara ili kudumisha uhusiano kati yao.
Pia huchunga mayai wanayotaga kwa zamu, huku jike wakielekea kukaa juu ya vifaranga wakati wa mchana na wanaume kuchukua zamu ya usiku. Vifaranga wanapoanguliwa, wazazi wote wawili pia hutoa chakula kwa watoto wao.
Chanzo - BBC SWAHILI
Social Plugin