Tanzia : MMILIKI WA ZAHANATI YA MITI MIREFU MJINI SHINYANGA Dkt. SAHAL AFARIKI DUNIA

Dkt. Mahamud Sahari enzi za uhai wake
Dkt. Mahamud Sahal enzi za uhai wake
**
Mmiliki wa Zahanati ya Miti Mirefu Mjini Shinyanga Dkt. Mahamud Sahal amefariki dunia leo Ijumaa Novemba 26,2021 baada ya kugongwa na pikipiki kwenye barabara iliyopo jirani na zahanati hiyo majira ya saa 12 jioni.

Inaelezwa kuwa Dr. Sahal amegongwa na pikipiki wakati akitoka katika zahanati akivuka barabara kuelekea kwenye kibanda cha Kahawa kilichopo upande wa pili wa barabara ambapo ghafla alitokea mwendesha bodaboda akiwa katika mwendo mkali na kumgonga.


“Dr. Sahal alikuwa anavuka barabara kuelekea kwenye kibanda cha kahawa ambacho mara kwa mara huenda anapopata nafasi lakini ghafla alitokea mwendesha bodaboda akitokea eneo la Nguzo Nane akiwa katika spiki kali, akamgonga mzee Sahal pamoja na mwanamke mmoja ambaye amejeruhiwa vibaya,amekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu lakini Dr. Sahal amefariki dunia majira ya saa 2 usiku”,wamesema mashuhuda wa tukio hilo.


“Mazishi ya Mwili wa Mzee wetu Dr. Sahal yatafanyika Jumamosi Tarehe 27/11/2021 saa 7 Mchana. Mzee Sahari ambaye nyumbani kwake ni Uzunguni mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga tutamkumbuka kwa kuupenda Mtaa wa Miti Mirefu hadi akaipa jina Hospitali yake Miti Mirefu. Ni Mzee aliyependa Umoja na Maendeleo ya Wana Miti Mirefu na Wanashinyanga kwa Moyo wa Upendo kabisa. 😭😭😭😭Pumzika kwa amani Dr. Sahal na Mwendo umeumaliza,Wanamtaa watakukumbuka na Historia umetuachia na tutaisimulia kwa wale tuliobaki, Nenda Baba”,amesema Mwenyekiti wa Mtaa wa Miti Mirefu Nassor Warioba.

R.I.P Dr. Sahal.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post