Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PINDA AKABIDHI MIFUKO ZAIDI YA 3,000 UJENZI OFISI ZA CCM BARIADI

Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Mizengo Kayanza Peter Pinda amekabidhi mifuko ya Saruji zaidi ya 3000 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za kata 31 iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mkoani Simiyu Mhandisi Kundo Andrea Mathew ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi aliyoitoa mapema baada ya kuchaguliwa.

Mifuko hiyo imekabidhiwa leo na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Mizengo Kayanza Peter Pinda mjini Bariadi ambapo kila kata imekabidhiwa mifuko ya saruji 100, mashine moja ya kufyatulia tofali ambapo pia Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Bariadi imekabidhiwa mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya katibu wa jumuiya hiyo.

Mhandisi Kundo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, ameambatana na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Bariadi na mkoa wa Simiyu.

Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Mizengo Peter Pinda akiwakabidhi makatibu kata pamoja na madiwani wa kata 31 za jimbo la Bariadi mifuko 100 ya saruji kwa kila kata pamoja na mashine moja kwa ajili ya kufyautilia tofali ahadi ambayo aliitoa mara baada ya kuwa Mbunge.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com