Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 blog Dodoma
Na Dotto Kwilasa, DODOMA.
ILI kuunga mkono juhudi za Serikali kwa vitendo katika kukuza uchumi kidigitali,Kampuni ya MhawaNet ICT imezindua duka la Teknolojia na Mawasiliano (TEHAMA)litakalo rahisisha huduma za mitandao huku ikiahidi kuongeza chachu ya ufanisi katika ubunifu wa utoaji wa huduma kwa Jamii na kufikia malengo ya uchumi wa pamoja.
Hatua hii imekuja kipindi ambacho Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inafanya jitihada kuhakikisha Taasisi zote za Serikali na binafsi zinaimarisha zaidi vitengo vya mawasiliano kwa Umma na mifumo ya utoaji elimu za mawasiliano ili kuboresha huduma kwa jamii.
Akiongea katika uzinduzi wa duka hilo uliofanyika Jijini Dodoma,Mkurugenzi wa MhawaNet ICT Saimon Chagula alisema,huduma hiyo itarahisisha Mawasiliano na kuwafanya Tanzania kuwa na ari ya kujiandaa kuingia katika hatua nzuri ya mapinduzi ya nne ya viwanda yatakayotoa mafanikio mazuri kwa uchumi.
"Mbali na huduma nyingi tunazotoa,Kampuni yetu itakuwa ikitoa ushauri wa matumizi bora na salama ya vifaa na mifumo ya TEHAMA,lakini pia tutatoa fursa ya ajira kwa vijana 30 ili kondokana tatizo la ajira kwa kuwa tunaamini unapompa ajira kijana mmoja unaongeza nguvu katika Taifa na kuwaondoa vijana katika wimbi la makundi mabaya,"amesema.
Amesema,ikiwa watanzania wengi watachochea maendeleo ya TEHAMA nchini, uchumi wa kijiditali utakua kwa kasi na kurahisisha huduma za mitandao ambapo hivi sasa vitu vingi hasa bili za maji, luku na malipo ya ardhi yanafanyika kwa njia ya mtandao.
"Kutokana na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia, TEHAMA imekuwa nguzo muhimu zaidi katika kuboresha utendaji kazi wa taasisi mbalimbali zikiwemo za umma,sasa tunaongeza kasi Kwa watu wa kawaida kuhakikisha wanaingia kwenye ulimwengu huu,"amesisitiza.
Chagula amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa janga la UVIKO 19 Teknolojia ya TEHAMA imesaidia watu kufanya mikutano kwa njia ya mtandao pamoja na shughuli mbalimbali za uagizaji mizigo nje ya nchi ikiwemo uagizaji wa vifaa mbalimbali hivyo ni Sekta muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Kwa upande wake Mtaalam wa masuala ya mtandao Serikalini,Daniel Roland Natai amepongeza ujio wa Kampuni hiyo ambapo amesema ni fursa kwa Wakazi wa Dodoma kwani itawapunguzia gharama za kusafiri hadi Dar es Salaam kufuta huduma hizo ikiwemo Kompyuta mpakato .
"Hapo awali wananchi wa Dodoma walikuwa wakisafiri kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kufuata huduma hizi za TEHAMA hivyo imewasaidia ,natoa wito kwa wakazi wa Dodoma kutumia Kampuni hii kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za TEHAMA,"amesema Natai.
Social Plugin