Waziri wa Maji Jumaa Aweso
Na Dotto kwilasa, Malunde 1 blog Dodoma
SERIKALI imesema katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara,wakazi wa mijini wanaopata huduma ya majisafi na salama imeongezeka kutoka asilimia 25 ya wakazi wote wanaoishi mijini mwaka 1961 hadi kufikia wastani wa asilimia 86 mwaka 2021.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso leo Jumatano Novemba 10,2021 wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wizara hiyo tangu kipindi cha uhuru na kuweka wazi kuwa Wizara hiyo imeendelea kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji katika maeneo ya mijini huku kwa upande wa vijijini kwa sasa ni wastani wa asilimia 72.3.
Amesema katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara,wastani wa wakazi wa mijini wanaopata huduma ya maji safi na salama imeongezeka kutoka asilimia 25 ya wakazi wote wanaoishi mijini mwaka 1961 hadi kufikia wastani wa asilimia 86 mwaka 2021.
Kuhusu upotevu wa maji,Waziri huyo amesema wamewasainisha mikataba Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji lengo likiwa ni kuzuia upotevu wa maji.
“Katika eneo la upotevu wa maji,Wizara imefanya mageuzi ambapo Wakurugenzi wetu tumewasainisha mkataba sio bla bla kwa mfano hili suala la upotevu wa maji unaweza ukapita kwenye Mamlaka za Maji anakwambia hapa tunapoteza maji kwa ni asilimia 48,kuna wiza wa maji baadhi ya hoteli hazilipi.
Tunaendelea kuwashguhulikia niombe sana si busara kuona maji yanamwagika halafu mwanananchi hana maji,”amesema.
Waziri huyo amesema Serikali imeendelea kuimarisha maabara za maji ili ziendelee kutoa huduma kama inavyokusudiwa.
Aidha,Waziri huyo amepiga marufuku ubambikizwaji wa bili za maji kwa wateja ambapo amedai ndiyo maana walianzisha Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)lengo likiwa ni kuondoa tatizo hilo.
“Kutokana na Ubambikizaji wa bili za maji ndiyo maana tulianzisha Ewura jukumu lake ni kudhibiti bili za maji tunawataka waendelee kufuatilia,ikitokea wakajulikana tutashughulika nao,”amesema.
"Mafanikio katika eneo la usimamizi wa ubora wa maji ni pamoja na Maabara ya Maji ya Mwanza iliteuliwa mwaka 2006 na Jumuiya ya Ulaya (EU) kupima ubora wa maji yanayotumika katika usindikaji wa minofu ya samaki kabla ya kusafirishwa kwenda katika soko la Ulaya na inaendelea na kazi hiyo,"ameongeza Waziri Aweso.
Social Plugin