Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DC KALLI AZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA, KONGAMANO LA BODABODA...KIVULINI YAMPONGEZA RAIS SAMIA WALIOPATA UJAUZITO KURUDI SHULE

Waendesha bodaboda wakiandamana wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Mkuu wa wilaya ya Magu Mkoani Mwanza Mhe. Salum Kalli akizungumza wakati akizindua Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yanayoongozwa na kauli mbiu ya ‘Ewe Mwananchi komesha ukatili wa kijinsia sasa’ leo Alhamisi Novemba 25,2021. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Magu Mkoani Mwanza Mhe. Salum Kalli amezindua Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yanayoongozwa na kauli mbiu ya ‘Ewe Mwananchi komesha ukatili wa kijinsia sasa’ huku akiwataka Waendesha bodaboda kujiepusha na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wa kike kwa vishawishi vya lifti na kuwa mabalozi wa kuwalinda wanafunzi hao.

Uzinduzi huo umefanyika leo Alhamisi Novemba 25,2021 katika ukumbi wa WAMA wilayani Magu wakati wa Kongamano la Waendesha Bodaboda lililoandaliwa na Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto KIVULINI ikiwa ni kundi linalolalamikiwa kujihusisha kimapenzi na wanafunzi na kuwapa mimba pamoja na kurubuni ‘kuchepuka’ na wake za watu.

Uzinduzi huo umeambatana na mdahalo uliowahusisha wanaharakati ngazi ya jamii, viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Magu, Jeshi la Polisi, Mahakama na waendesha bodaboda 100 lengo likiwa kujengeana uelewa ili kwa pamoja wadau hao washirikiana kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.

Mkuu huyo wa wilaya amewahimiza waendesha bodaboda ambao ni miongoni kujiepusha na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wa kike kutokana na kudaiwa kwamba wamekuwa wakiwashawishi kuwapa lifti wakati wa kwenda ama kutoka shule na kuwapa zawadi zikiwemo chips.

“Jamii haipaswi kunyamazia vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vipigo kwa wanawake, kujihusisha kimapenzi na wanafunzi, mimba na ndoa za mapema. Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ametuletea fedha shilingi bilioni 2.46 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 123 vya madarasa katika Shule za Sekondari, tusipowalinda wanafunzi mnataka akasome nani kwenye hayo madarasa? Tushirikiane ili tuhakikishe wanatimiza ndoto zao", amesema Kalli.

Kalli amewaonya baadhi ya watendaji katika vyombo vya utoaji maamuzi kuchelewesha kesi zinazohusiana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo mimba kwa wanafunzi wa kike kwa kisingizio cha upelelezi kutokamilika na kusababisha kesi hizo kutopata mafanikio.

"Mwanafunzi anapewa ujauzito, anamtaja aliyempa huo ujauzito, mnamkamata lakini kesi haifiki mwisho hadi anajifungua na mtoto anaanza shule huku bado kesi haijaisha kwa madai upelelezi haujakamilika, hii hapana, acheni kukwamisha kesi hizi. Naomba madawati ya Jinsia yatusaidie kwa sababu wakati mwingine kesi zinachukua muda mrefu, upelelezi kila siku wakati mambo yote yapo wazi", amesema Kalli.

Katika hatua nyingine amesema kila mmoja katika jamii ana wajibu wa kulinda wanawake na watoto akisisitiza kuwa mwanamke ana haki na uwezo wa kufanya jambo lolote katika jamii kama ilivyo kwa wanaume.

“Tuwalinde na kuwatunza wanawake, tusilete mzaha. Tuwape haki ya elimu,tusiwape mimba watoto wa kike,wanawake wapewe haki ya kumiliki mali. Na nyinyi waendesha bodaboda mnayo nafasi kubwa sana ya kuleta mabadiliko”,amesema Kalli.

Kalli ametumia fursa hiyo kulipongeza shirika la KIVULINI kwa namna linavyoshirikiana na serikali katika kutokomeza mimba za utotoni, ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto akieleza kuwa kutokana na elimu ambayo imekuwa ikitolewa naa shirika hilo matukio ya ukatili yameanza kupungua katika jamii.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally amesema katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia 2021, shirika hilo litaendesha shughuli mbalimbali ikiwemo midahalo ili kuendelea kuhamasisha jamii kupinga na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa katika kutokomeza mimba za utotoni, ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

"Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia huadhimishwa kila mwaka kuanzia tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Disemba.Tumeona ni vyema kukutana na waendesha bodaboda kwani ni kundi ambalo limekuwa likituhumiwa kuwa baadhi yao wanawapa mimba wanafunzi na kutembea ‘kuchepuka’ na wake za watu. Tunataka wawe mawakala/mabalozi wa mabadiliko. 

Tumewapa pia Reflectors ‘Viaksi mwanga’. Tunaamini kupitia waendesha bodaboda hawa jamii itapata elimu hivyo kutokomeza mimba za utotoni, ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto”,amesema Ally.

"Ni jukumu la kila mmoja wetu kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia. Mwanaume Chapa Kazi, Sio Mkeo, Kama unapenda sketi za shule mshonee mkeo, ikiwezekana weka marinda na kengele kabisa. Funguka Muwezeshe asome usimpe mimba",amesema Ally.

Ally amewataka wazazi kuacha kulaza watoto na wageni ili kuepusha na matukio ya ukatili kwani matukio mengi yanafanywa na watu wa karibu.

 "Pia natoa wito kwa Shule za Msingi na Sekondari na Mamlaka za Elimu nchini kwa kuanzisha klabu na madawati ya kushughulikia masuala ya ukatili wa kijinsia na kuweka mifumo ya kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia mashuleni",amesema Ally.

Kwa upande wake, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Faraja Mkinga kutoka Kitengo cha Dawati la Jinsia Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza amesema jeshi la polisi limeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kutokomeza vitendo vya ukatili katika jamii ikiwemo kutoa elimu na kushughulikia kesi zinazohusu matukio ya ukatili wa kijinsia.

Mkurugenzi huyo wa Shirika la KIVULINI lenye makao makuu Nyamhongolo jijini Mwanza ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuruhusu wanafunzi waliopata ujauzito kuendelea na masomo yao katika mfumo ulio rasmi akieleza kuwa  uamuzi huo una tija.

"Uamuzi huu wa serikali una tija kubwa lakini naomba jamii na serikali ziongeze nguvu katika kutoa elimu ya stadi za watoto wa kike kujitambua,kujilinda na kufikia ndoto zao kielimu na kuimarisha malezi na ulinzi na usalama wa  watoto wawapo shuleni, kwenye jamii na majumbani",amesema Ally.

Mkinga amesema kesi nyingi za matukio ya ukatili wa kijinsia zimeendelea kupata mafanikio mfano kesi 84 za ukatili wa kijinsia kwa mwaka 2020 zilipata mafanikio huku kesi 48 zikipata mafanikio kwa mwaka 2021 kuanzia mwezi Januari hadi Novemba na hatua za kisheria kuchukuliwa kwa wahusika.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu, Faustine Makingi amelishukuru Shirika la KIVULINI amewataka waendesha bodaboda kuwa mabalozi wazuri wa kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia akisema hategemei kuona waendesha bodaboda wanafanya matukio ya ukatili wa kijinsia huku akiwahamasisha kuchangamkia mikopo inayotolewa katika halmashauri.

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mwanza, Isack Ndassa
amesema asilimia 90 ya waendesha bodaboda ni wanaume, asilimia 90 ya wateja wao ni wanawake hivyo wanalo jukumu kubwa ni kuwalinda wanawake na kuwa tayari kuleta mabadiliko katika jamii.

Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda Kanda ya Magu Mjini, Walter Yewa na Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda Wilaya ya Magu Mudy Jumanne Masoud wamelishukuru na kulipongeza shirika la KIVULINI kwa kutoa elimu ya masuala ya ukatili wa kijinsia na kuomba elimu hiyo endelevu.

"Tunaliomba Jeshi la Polisi muwe na siri, sisi tunakutana na mambo mengi sana,tuna taarifa nyingi ya matukio ya uhalifu na matukio mengine ya ajabu ajabu lakini tunapotoa taarifa baadhi ya askari siyo waaminifu, wanatoa siri. Kwa pamoja tutamaliza matukio ya ukatili wa kijinsia kama tutashirikiana", wamesema.

Wakizungumza katika uzinduzi huo, Waendesha bodaboda wamezitaja baadhi ya sababu za baadhi yao kujihusisha kimapenzi na wanafunzi na wake za watu kuwa ni vishawishi wanavyokumbana navyo ikiwemo mavazi mabaya yanayoacha mwili wazi na tamaa.

“Kamserereko kanachangia mimba za wanafunzi, wanafunzi wanapenda vitu vya bure, bodaboda nao wanataka wanawake wa gharama nafuu, kamserereko haka pia kanaangukia kwa wake za watu, watoto wa kike wanapenda kubebwa bure na kutushika shika matokeo yake hisia zinatushinda tunaangukia kwenye mapenzi, tunaombwa sana fedha za chai na soda matokeo yake na sisi tunaamua kujilipa. Hivi sasa tumejitambua tutaepuka majaribu haya”, amesema mmoja wa waendesha bodaboda hao.

Hata hivyo waendesha bodaboda hao wamesema kutokana elimu inayotolewa na shirika la KIVULINI wamejitambua na kuahidi kuwa sehemu ya mabadiliko katika kumlinda mtoto wa kike.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Magu Mkoani Mwanza Mhe. Salum Kalli (katikati) akiwasili katika ukumbi wa WAMA kwa ajili ya kuzindua Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yanayoongozwa na kauli mbiu ya ‘Ewe Mwananchi komesha ukatili wa kijinsia sasa’ leo Alhamisi Novemba 25,2021. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Magu Mkoani Mwanza Mhe. Salum Kalli akizungumza wakati akizindua Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yanayoongozwa na kauli mbiu ya ‘Ewe Mwananchi komesha ukatili wa kijinsia sasa’ leo Alhamisi Novemba 25,2021. 
Mkuu wa wilaya ya Magu Mkoani Mwanza Mhe. Salum Kalli akizungumza wakati akizindua Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yanayoongozwa na kauli mbiu ya ‘Ewe Mwananchi komesha ukatili wa kijinsia sasa’ leo Alhamisi Novemba 25,2021. 
Mkuu wa wilaya ya Magu Mkoani Mwanza Mhe. Salum Kalli akizungumza wakati akizindua Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yanayoongozwa na kauli mbiu ya ‘Ewe Mwananchi komesha ukatili wa kijinsia sasa’ leo Alhamisi Novemba 25,2021. 
Mkuu wa wilaya ya Magu Mkoani Mwanza Mhe. Salum Kalli akizungumza wakati akizindua Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yanayoongozwa na kauli mbiu ya ‘Ewe Mwananchi komesha ukatili wa kijinsia sasa’ leo Alhamisi Novemba 25,2021. 
Mkuu wa wilaya ya Magu Mkoani Mwanza Mhe. Salum Kalli akizungumza wakati akizindua Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yanayoongozwa na kauli mbiu ya ‘Ewe Mwananchi komesha ukatili wa kijinsia sasa’ leo Alhamisi Novemba 25,2021. 
Mkuu wa wilaya ya Magu Mkoani Mwanza Mhe. Salum Kalli akizungumza wakati akizindua Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yanayoongozwa na kauli mbiu ya ‘Ewe Mwananchi komesha ukatili wa kijinsia sasa’ leo Alhamisi Novemba 25,2021. 
Waendesha bodaboda wakiwa kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yanayoongozwa na kauli mbiu ya ‘Ewe Mwananchi komesha ukatili wa kijinsia sasa’ leo Alhamisi Novemba 25,2021. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yanayoongozwa na kauli mbiu ya ‘Ewe Mwananchi komesha ukatili wa kijinsia sasa’ leo Alhamisi Novemba 25,2021. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akitoa elimu ya masuala ya ukatili wa kijinsia wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yanayoongozwa na kauli mbiu ya ‘Ewe Mwananchi komesha ukatili wa kijinsia sasa’ leo Alhamisi Novemba 25,2021. 

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mwanza, Isack Ndassa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu, Faustine Makingi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda Kanda ya Magu Mjini, Walter Yewa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda Wilaya ya Magu Mudy Jumanne Masoud akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Inspekta Oscar Msuya kutoka Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Faraja Mkinga kutoka Kitengo cha Dawati la Jinsia Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza akitoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Magu, Amandus Mboya akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Inspekta Msafiri  Akilimali kutoka Kituo cha Polisi wilaya ya Magu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Hakimu Mkazi Mahakam ya wilaya ya Magu, Erick Kimaro akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Afisa Maendeleo ya Jami ngazi ya wilaya ya Magu, Shida Missana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Muonekano wa sehemu ya pikipiki za waendesha bodaboda wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Waendesha bodaboda wakiwa wamevaa viaksi mwanga vilivyotolewa na Shirika la KIVULINI wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Waendesha bodaboda wakiandamana wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Waendesha bodaboda wakiandamana wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Waendesha bodaboda wakiandamana wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Waendesha bodaboda wakiandamana wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Waendesha bodaboda wakiwa wamevaa viaksi mwanga vilivyotolewa na Shirika la KIVULINI wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Wana Mabadiliko wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Waendesha bodaboda wakiwa wamevaa viaksi mwanga vilivyotolewa na Shirika la KIVULINI wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Waendesha bodaboda wakiwa wamevaa viaksi mwanga vilivyotolewa na Shirika la KIVULINI wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Mwendesha bodaboda Ibrahim Samwel akizungumza  wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Mwendesha bodaboda akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.

Wana mabadiliko wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.
Waendesha bodaboda wakiwa wamevaa viaksi mwanga vilivyotolewa na Shirika la KIVULINI wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Magu mkoani Mwanza.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com