Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Nicolaus Herman Shombe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Shombe alikuwa Kamishna wa Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango.
Dkt. Shombe anachukua nafasi ya marehemu Prof. Damian Gambagambi ambaye alifariki akiwa katika nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 2, 2021 na Jaffar Haniu ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu imeeleza kuwa, uteuzi huo umeanza tarehe 29 Oktoba, 2021.
Social Plugin