Watoto 25 wenye umri kati ya miaka mitano na sita wamefariki dunia Novemba 9, 2021 baada ya darasa lao lililojengwa kwa mbao na makuti kuungua moto nchini Niger.
Meya wa Jiji la Maradi, Chaibou Aboubacar, amesema Watoto 13 wamejeruhiwa na wanne kati yao hali zao ni mbaya.
Ajali hiyo ilitokea wakati watoto wakiwa darasani na bado chanzo cha moto huo ulioteketeza madarasa matatu bado hakijafahamika na kwa sasa Shule imefungwa kwa muda.
Itakumbukwa Mwezi April mwaka huu Watoto wengine 20 walifariki kwa kuungua moto pia wakiwa darasani katika Wilaya ya Niamey nchini humo.
Social Plugin