MOJA ya taarifa za kusikitisha iliyotolewa jana ni ile inayohusu mwanaume mmoja Jijini Mbeya amejichoma kwa moto mwili mzima hadi kufa huku sababu ya kufanya hivyo ikitajwa kuwa ni msongo wa mawazo kutokana na kukimbiwa na mke wake.
RPC Mbeya Ulrich Matei amesema; “Tarehe Novemba 8, mwaka huu saa tatu asubuhi kwenye Kijiji cha Ihombe, Mbeya Vijijini Mwanaume huyo aitwae Mashaka Simon Yokonia (35) alikutwa ndani ya nyumba yake akiwa amejiunguza moto”
“Alijiunguza moto, kabla ya hili tukio amekua akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na alitelekezwa na Mke wake hali iliyomfanya kukata tamaa ya maisha, siku chache zilizopita alifanya pia jaribio la kujilipua na petroli kabla ya kuokolewa na Mdogo wake,” amesema RPC Matei.
Social Plugin