Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ASAKWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI, WEZI SUGU WA PIKIPIKI WADAKWA


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia wahamiaji haramu saba [07] raia wa nchini Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.

Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 20.11.2021 majira ya saa 12:00 asubuhi huko Igawa – Check Point, Kata ya Lugelele, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya. Wahamiaji waliokamatwa ni 1. IZACK FEISAL [22], 2. LAMATO IBRAHIM [18], 3. NASANDAT DILEN [23], 4. KELVIN LOLANJE [30], 5. ANDAMAYO ABABALA [20], 6. ZENA GAMOLO [20] na 7. JASO BONKARA [19] wote raia wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali. Taratibu za kuwasiliana na idara ya uhamiaji kwa hatua zaidi za kisheria zinaendelea.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA WIZI WA MIFUGO.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili 1. MAJALIWA ANYELWISYE [25] Mkazi wa Sokomatola – Mbeya na 2. ALEX OMARY [27] Mkazi wa Uyole Kati – Mbeya wakiwa na Ng’ombe mmoja Jike mali ya wizi.

Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 20.11.2021 majira ya saa 03:15 Asubuhi huko maeneo ya Katumba, Kata ya Ibighi, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya baada ya kufanyika msako na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa na Ng’ombe huyo waliyemuiba Kijiji cha Lubanda nyumbani kwa JONAS MWAMBENE [72] Mkazi wa Lubanda wakiwa katika harakati za kwenda kumuuza Katumba – Rungwe.

KUPATIKANA NA MALI YA WIZI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia ASIFIWE GODWIN MWAMPOMBE [23] Mkazi wa Ndandalo – Kyela akiwa na mali ya wizi Pikipiki Na.T.80 CSS Kinglion rangi nyekundu.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 21.11.2021 majira ya saa 01:30 usiku huko Kitongoji cha Kampunga, Kata ya Njisi, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya na katika mahojiano alishindwa kuonyesha nyaraka zozote zinazoonesha uhalali wa kuwa na Pikipiki hiyo.

KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA WA MAUAJI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia SHIZYA JUMA @ RAIS [32] Mkazi wa Kijiji cha Mbagala kwa tuhuma za tukio la mauaji ya CLEMENCE SALIMO [40] Mkazi wa Mbawi.

Ni kwamba mnamo tarehe 16.11.2021 huko Kijiji cha Mbawi kilichopo Kata ya Ilembo, Tarafa ya Isangati, Wilaya ya Mbeya CLEMENCE SALIMO [40] Mkazi wa Mbawi alikutwa kwenye mashamba ya Kwamela akiwa amefariki dunia baada ya kukatwa kwa kitu chenye ncha kali usoni, kifuani na shingoni na mtu/watu wasiofahamiaka.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoani hapa lilianza msako kufuatia taarifa za raia wema na mnamo tarehe 21.11.2021 lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa tukio hilo la mauaji ambaye mara baada ya kutekeleza tukio hilo alikimbia na kwenda kujificha huko Kijiji cha Ilomba, Kata ya Iyula, Tarafa ya Iyula, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe.

Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

KUKAMATWA KWA WEZI SUGU WA PIKIPIKI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili 1. MUGANYIZI VICTOR LEOPORD [36] Mkazi wa Ngokolo na 2. MAJALIWA MWASHUYA [31] Mkazi wa Sogea – Tunduma Mkoa wa Songwe kwa tuhuma za wizi wa Pikipiki yenye namba za usajili MC.810 CCH Kinglion.

Ni kwamba mnamo tarehe 21.11.2021 majira ya saa 11:30 Alfajiri huko katika Msitu wa Hifadhi wa Mbiwe uliopo Kata ya Makongolosi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la GODLUCK ANDENGULILE [22] Mchimbaji Madini na Mkazi wa Matundasi akiwa anatoka kwenye kazi ya uchimbaji alivamiwa na watuhumiwa ambao walikuwa wamevalia sare za JWTZ na kumpora Pikipiki yake MC.810 CCH Kinglion.

Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilianza msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa MUGANYIZI VICTOR LEOPORD [36] Mkazi wa Ngokolo na 2. MAJALIWA MWASHUYA [31] Mkazi wa Sogea – Tunduma. Katika upekuzi mtuhumiwa MUGANYIZI VICTOR LEOPORD alikutwa na cheti cha JKT chenye Na.AD.9664 SM MUGANYIZI VICTOR LEOPORD amemaliza mafunzo 25/06/2009 Kikosi cha Kanembwa.

Watuhumiwa wamehojiwa na kukiri kuhusika kwenye tukio hilo. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

ASAKWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamsaka mtuhumiwa aliyefahamika kwa jina la SKACHA, mkazi wa Kitongoji cha Kasakalawe, Wilaya ya Chunya kwa tuhuma za mauaji ya ADAM JACOB [31] Mchimbaji Madini na Mkazi wa Kasakalawe.

Ni kwamba mnamo tarehe 21.11.2021 majira ya saa 04:30 usiku huko Kitongoji cha Kasakalawe, Kata ya Matundasi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. ADAM JACOB [31] alijeruhiwa kwa kuchomwa kitu chenye ncha kali mgongoni na SKACHA na alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu Zahanati ya LIOCHI iliyopo Mji Mdogo – Makongolosi.

Chanzo cha tukio ni wivu wa kimapenzi ambapo mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mpenzi wake. Msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa unaendelea.

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com