Daktari wa mifugo wa kijiji cha Loiborsoit A wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara, Malipe Ole Kisota ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu waliomtuhumu kumpa mimba mke wa ndugu yao.
Imeelezwa kuwa alikatwa na sime sehemu mbalimbali mwilini na ndugu watatu, Lazaro, Mamei na Supek Mamei, wakimtuhumu kumpa ujauzito mke wa ndugu yao Kinaruu Mamei.
Kamanda Mwakyoma amesema chanzo cha kifo hicho ni wivu wa mapenzi, akidai marehemu alikuwa akituhumiwa kutembea na mke wa mtu na alikuwa anatafutwa akawa anajificha na siku ya tukio walimkimbiza, kumkamata na kufanya mauaji hayo.
SOMA ZAIDI <<HAPA>>
Via Mwananchi
Social Plugin