Zoezi la kuchinja ng'ombe likiendelea wakati wa uzinduzi wa Machinjio ya Kisasa ya ng’ombe na mbuzi yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amezindua Machinjio ya Kisasa ya ng’ombe na mbuzi yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga huku akitoa agizo kwa Wachinjaji katika mitaa mbalimbali Mjini Shinyanga kuhamia katika machinjio hayo mapya ambayo yanafuata taratibu zote za afya.
Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatatu Novemba 22,2021 na kuhudhuriwa na viongozi na wananchi wa Manispaa ya Shinyanga waliokuwa na kiu kubwa ya kuona machinjio hiyo inaanza kufanya kazi ili wapate fursa mbalimbali pamoja na kupata kitoweo kilichoandaliwa katika mazingira safi na salama.
“Tumezindua Machinjio haya kwa kuchinja ng’ombe wanne leo,hatukuwahi kufanya uchinjaji lakini baada ya kufanya zoezi hili tumebaini uwepo wa changamoto za kitaalamu hali inayosababisha leo zoezi litumie muda mrefu.Tutarekebisha changamoto zilizojitokeza na kesho Jumanne Novemba 23 tutaanza rasmi uchinjaji ambapo kazi itafanyika kwa kasi zaidi”,amesema Mboneko.
“Naomba tutumie machinjio haya kwani nyama inayotoka hapa itakuwa na ubora mkubwa iliyoandaliwa katika mazingira bora yanayozingatia kanuni na taratibu za afya. Machinjio zote zilizopo huko mtaani tunazifunga wiki hii ili wachinjaji wote wahamie hapa”,amesema Mboneko.
Mkuu huyo wa wilaya pia amesisitiza matumizi ya magari katika kusafirisha nyama badala ya kutumia matoroli na mifuko ili kuhakikisha nyama zinakuwa salama na bora kwa matumizi ya binadamu.
Aidha amewakaribisha wafanyabiashara wa ng’ombe na mbuzi ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga kutumia machinjio hiyo kuchinja mifugo na kusafirisha nyama badala ya kusafirisha wanyama wakiwa hai.
Mboneko amewahamasisha wakazi wa eneo la Ndembezi kuchangamkia fursa zinazopatikana katika machinjio hayo ikiwemo ajira zisizo za kitaalamu huku akiwasisitiza kuwa waadilifu na waaminifu kwa kufika kazini kwa wakati na kuepuka udokozi wa nyama katika machinjio hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura amesema mpaka sasa mradi huo wa Machinjio ya Kisasa umegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 5.2 huku akieleza kuwa mradi huo ulichelewa kuanza kutokana na changamoto ya Mfumo wa Majitaka na Mfumo wa Ubaridi (Cold Room) na baada ya kuzitatua uchinjaji umeanza na wanategemea kuchinja kwa kasi zaidi kuanzia kesho Jumanne.
Mwenyekiti wa Wachinjaji mkoa wa Shinyanga, Masaka Charles amesema kutokana na kuzinduliwa kwa machinjio hiyo wachinjaji wote Mjini Shinyanga watahamia hapo ili kuendesha shughuli za uchinjaji.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cham Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mhe. Abubakar Mukadam amesema machinjio hiyo imeanza kufanya kazi baada ya serikali kutatua changamoto zilizokuwepo huku akitaka siasa kutoingizwa kwenye mradi huo.
Diwani wa kata ya Ndembezi Mhe. Victor Mmanywa ameshukuru kuzinduliwa kwa machinjio hiyo ambayo itawezesha wakazi wa kata ya Ndembezi kupata fursa mbalimbali.
Nao wakazi wa Ndembezi wameeleza kufurahishwa na kuanza kazi kwa machinjio hiyo wakisema matumaini yao ni kupata fursa za ajira.
Hata hivyo baadhi ya watu waliohudhuria uzinduzi huo wameeleza kushangazwa na zoezi la uchinjaji lilivyoendeshwa kwa kutumia mikono badala ya kutumia mitambo kama walivyokuwa wameelezwa na kusababisha zoezi la kuchinja ng'ombe wanne lichukue zaidi ya saa moja ambapo majibu yaliyopatikana ni kwamba waliamua kuchinja na kuendesha zoezi zima la uchinjaji kwa mikono kutokana na sababu za kitaalamu kwani anayepaswa kuwasha mtambo wa machinjio hakuwepo.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Ng'ombe wakipelekwa eneo la kuchinjia katika Machinjio ya Kisasa ya ng’ombe na mbuzi yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga leo Jumatatu Novemba 22,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Ng'ombe akichinjwa katika Machinjio ya Kisasa ya ng’ombe na mbuzi yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga leo Jumatatu Novemba 22,2021.
Zoezi la uchinjaji ukiendelea katika Machinjio ya Kisasa ya ng’ombe na mbuzi yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga leo Jumatatu Novemba 22,2021.
Ng'ombe wakichunwa kwa visu katika Machinjio ya Kisasa ya ng’ombe na mbuzi yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga leo Jumatatu Novemba 22,2021.
Viongozi na wananchi wakishuhudia Ng'ombe wakichunwa katika Machinjio ya Kisasa ya ng’ombe na mbuzi yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga leo Jumatatu Novemba 22,2021.
Viongozi na wananchi wakishuhudia zoezi la uchinjaji katika Machinjio ya Kisasa ya ng’ombe na mbuzi yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga leo Jumatatu Novemba 22,2021.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwa katika gari la kubebea nyama katika Machinjio ya Kisasa ya ng’ombe na mbuzi yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga leo Jumatatu Novemba 22,2021.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akiwa katika eneo la Mfumo wa Ubaridi 'Cold Room' akielezea jinsi nyama zitakavyohifadhiwa kabla ya kusafirishwa nje ya mkoa wa Shinyanga
Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akielezea namna Mfumo wa Mfumo wa Maji taka unavyofanya kazi katika machinjio ya kisasa ya Ndembezi
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura (mwenye tisheti nyeusi) akielezea namna Mfumo wa Mfumo wa Maji taka unavyofanya kazi katika machinjio ya kisasa ya Ndembezi
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akizindua Machinjio ya Kisasa ya ng’ombe na mbuzi yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akizindua Machinjio ya Kisasa ya ng’ombe na mbuzi yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa akizindua Machinjio ya Kisasa ya ng’ombe na mbuzi yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akizungumza wakati wa uzinduzi wa Machinjio ya Kisasa ya ng’ombe na mbuzi yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Wachinjaji mkoa wa Shinyanga, Masaka Charles akizungumza wakati wa uzinduzi wa Machinjio ya Kisasa ya ng’ombe na mbuzi yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga
Diwani wa kata ya Ndembezi Victor Mmanywa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Machinjio ya Kisasa ya ng’ombe na mbuzi yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga
Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha Manispaa ya Shinyanga, Hassan Mwendapole akizungumza wakati wa uzinduzi wa Machinjio ya Kisasa ya ng’ombe na mbuzi yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Esther Makune akizungumza wakati wa uzinduzi wa Machinjio ya Kisasa ya ng’ombe na mbuzi yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Chama Cham Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mhe. Abubakar Mukadam akizungumza wakati wa uzinduzi wa Machinjio ya Kisasa ya ng’ombe na mbuzi yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga
Social Plugin