Ziara katika Chemchemi ya Maji ya Kimaya, Mto Chepkulo kaunti ya Bomet nchini Kenya imegeuka kuwa mauti baada ya mwanafunzi mwenye umri wa miaka 24, kuzama akipiga picha.
Katika kisa hicho cha Jumapili, Oktoba 31,2021 mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Bomet alikuwa amesonga katika eneo la kina kirefu kupiga picha bora zaidi kabla ya kubebwa na mawimbi ya chemchemi ya maji hayo.
Akithibitisha kisa hicho, Mkuu wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Chepalungu, Nelson Masai alisema mwanafunzi huyo wa kiume wa mwaka wa pili alikuwa amezuru eneo hilo pamoja na marafiki zake wengine 12.
Masai aliongezea kuwa marehemu pamoja na wenzake huenda walipuuza kina cha mto huo na kuamua kujiharatisha,Citizen iliripoti.
Wanafunzi ambao walikuwa wameandamana na marehemu bado hawajatambuliwa lakini wanasakwa na polisi kuandikisha taarifa. Bado mwili wa mwanafunzi huyo haujapatikana licha ya msako wa wapiga mbizi wa Bomet kutafuta kila mahali.
Chanzo - Tuko News
Social Plugin