Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linamshikilia mtu mmoja mwenye umri wa miaka 25 (jina limehifadhiwa) mkazi wa mtaa wa Ilazo jijini Dodoma kwa tuhuma za kumbaka mwanamke mjamzito mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa mtaa wa Kisasa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 22, 2021 jijini Dodoma kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Onesmo Lyanga amesema kuwa tukio hilo limetokea Novemba 20, 2021 majira ya saa kumi alfajiri huko mtaa wa kisasa kata Makulu jijini Dodoma.
Kamanda Lyanga amesema kuwa chanzo cha tukio hilo ni tamaa za kimwili ambapo mtuhumiwa alimvamia mwanamke huyo akiwa amelala na kumfanyia kitendo hicho kilichompelekea kupata maumivu makali.
“Alimbaka Mama mjamzito kwa visingizio mbalimbali aidha vya ulevi, sijui nilipotea mlango lakini suala ni kwamba kosa la ubakaji limefanyika, yeye aendelee kutoa utetezi wake lakini sisi tunachukua sheria muda si mrefu atafikishwa katika vyombo vya sheria” amesema Kamanda Lyanga.
Social Plugin