Diwani wa kata ya Chamaguha Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akila kiapo kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga . Picha na Amos John
***
Diwani wa kata ya Chamaguha Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko ameapishwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga baada ya kuchaguliwa kwa kura za Ndiyo na Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021.
Masumbuko amepigiwa kura 20 za Ndiyo kati ya kura zote 20 zilizopigwa wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichohudhuriwa pia Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko pamoja Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi, Gerald Mwaitebele.
Akizungumza baada ya kuapishwa kuwa Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Masumbuko ameahidi kushirikiana na madiwani na watendaji wa halmashauri kuboresha ukusanyaji mapato, kusimamia miradi ya maendeleo, kudhibiti mianya ya rushwa ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Shinyanga umefanyika kufuatia aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Mathew Nkulila kufariki dunia Agosti 23,2021.
Diwani wa kata ya Chamaguha Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akiapa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021. Kulia ni Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi, Gerald Mwaitebele. Picha na Amos John
Diwani wa kata ya Chamaguha Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akiapa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021. Kulia ni Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi, Gerald Mwaitebele.
Kulia ni Diwani wa kata ya Chamaguha Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akienda kubadilisha Joho la Udiwani ili avae Joho la Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021.
Diwani wa kata ya Chamaguha Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akizungumza baada ya kuapishwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021.
Diwani wa kata ya Chamaguha Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akizungumza baada ya kuapishwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati Diwani wa kata ya Chamaguha Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akiapishwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021.
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akimkabidhi Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko Kanuni za Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021.
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akimkabidhi Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko Kanuni za Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021.
Kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu akimkabidhi Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko Ilani ya CCM leo Jumanne Novemba 30,2021.
Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi, Gerald Mwaitebele amekabidhi Sheria ya Maadili na Kanuni za Maadili Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko baada ya kuapishwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Esther Makune akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani leo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Jomaari Mrisho Satura akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021.
Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Nassor Warioba akizungumza kwenye Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021.
Diwani wa Kata ya Kambarage Hassan Mwendapole akitoa neno la shukrani kwa niaba ya madiwani baada ya Diwani wa kata ya Chamaguha Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko kuapishwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Luther Mneney akizungumza baada ya Diwani wa kata ya Chamaguha Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko kuapishwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021.
Mfanyabiashara Maarufu Gilitu Makula akizungumza baada ya Diwani wa kata ya Chamaguha Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko kuapishwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 30,2021.
Wageni mbalimbali wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani Manispaa ya Shinyanga.
Picha zote na Amos John