Mtu mmoja amepoteza maisha na watatu kujeruhiwa kutokana na mvua kubwa zilizonyesha kuanzia siku ya tarehe 2 hadi 3 Novemba, mwaka huu katika wilaya za Momba na Ileje Mkoani Songwe.
Mvua hizo zilizoambatana na upepo mkali zimesababisha pia maafa makubwa ikiwemo kubomoa na kusomba nyumba 46 za wakazi wa eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba amewatembelewa wahanga hao na kuwapa pole akisema kuwa nyumba 36 zimebomolewa katika wilaya ya Ileje na 10 katika wilaya ya Momba huku akitaja kuwa chanzo cha mvua hizo ni mabadiliko ya tabia ya nchi yanayotokana na shughuli za kibinadamu.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey M. Kasekenya, amekutana na viongozi wa Kijiji Cha Yuli kata ya Mlale kutathmini kutathmini madhara yaliyotokana na Mvua zilizoambatana na upepo mkali na kusababisha Nyumba 36 kuezuliwa na kifo cha mtu mmoja.