Na Mwandishi Maalum, Dodoma
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Dkt Eliezer Feleshi amemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kumuamini na kumteua katika nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Dkt Feleshi ametoa shukrani hizo leo( Alhamisi) Jijini Dodoma, akisimama kwa mara ya kwanza mbele ya Bunge hilo tangu alipoteuliwa kuwa AG na baada ya kula kuiapo cha uaminifu kwa Bunge hilo, wakati alipokuwa akiwasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali ( Na 6) wa mwaka 2021 katika Mkutano wa Tano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru sana Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania kwa kuniamini na kuniteua katika nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.” Akasema AG Feleshi
Na kuongeza “ Ninamuahidi kutekeleza majukumu yangu haya mapya kwa weledi, umahiri na uamininifu mkubwa”.
“Pili nimshukuru Mungu tena kwa kuniwezesha kusimama kwa mara ya kwamba mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ( Na 6) wa Mwaka 2021” akasema Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Akiwasilisha Muswada huo wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ( Na 6) wa mwaka 2021 ( The Written Laws ( Miscelaneous Amendiments) No (6), Bill.2021, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema Muswada huo unapendekeza marekebisho katika sheria zifuatazao;
Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya 332; Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya 438 na Sheria ya Kodi la Ongezeko la Thamani, Sura ya 148.
Kwa mujibu wa AG Feleshi, Muswada aliouwalisha mbele ya Bunge, umegawanyika katika sehemu Nne ambapo sehemu ya kwanza ya Muswada inaainisha masharti ya utagulizi, ikiwa ni pamoja na jina la Sheria pendekezwa na tamko la marekebisho ya sheria mbalimbali zinazokusudiwa kufanyiwa marekebisho kupitia Muswada huo.
Akalieleza Bunge hilo kwamba, sehemu ya pili ya Muswada huo inapendekeza marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya 332, ambapo kifungu cha 83B kinapendekeza kufutwa kwa lengo la kuondoa kodi ya zuio ya asilimia mbili kwa mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji.
“Lengo la marekebisho ya haya ni kulinda vipato vya wakulima kwa kuwapunguzia mzigo unaotokana na utozwaji wa kodi” amebainisha Dkt. Feleshi.
Kuhusu sehemu ya tatu ya Muswada, ikisomwa pamoja na Jedwali la marekebishoa ya Serikali , inapendekeza marekebisho katika Sheria ya Usimamizi wa kodi Sura ya 438 ili kurekebisha kifungu cha 7 kwa kuongeza kufungu kidogo cha 3.
“Marekebisho hayo yanalenga kutambua Mkataba wa utekelezaji wa Mradi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda kwenda Chongoleani Tanga ili utekelezaji wa sheria za kodi usiathiri masharti mahususi ya mkataba huo kama ilivyokubaliwa na pande zote
Kuhusu sehemu ya Nne ya Muswada huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema, upande wa sehemu ya Nne ya Muswada inayopendekeza marekebisho ya kufuta sheria ya kodi ya ongezeko la thamani Sura ya 148, inapendeleza kufutwa. “ Hatua hiyo inatokana na mashauriano ya kina kati ya Serikali na Kamati
WAKATI HUO HU, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Feleshi, amewapongeza watumishi wote wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakiongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt, Evaristo Longopa kwa kuendelea kutekeleza majukumu na kazi za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ikiwamo kuandaa Muswada huo na ambao umesimamiwa kwa karibu na Bw, Onorius Njole, Mwandishi Mkuu wa Sheria akishirikiana na Waandishi wa Sheria wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
“ Tunatambua na tutaendelea kutekeleza majukumu yetu kwa weledi, ufanisi na kuweka mbele maslahi ya nchi yetu” amesisitiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Feleshi.