Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba
WAZIRI wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema kuwa Tanzania ina jumla ya mabilionea 5,740 wanomiliki asilimia 4.2 ya utajiri wa mabilionea barani Afrika, huku akibainisha kuwa tayari wameshasajiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA.
Mwigulu amesema haya leo Novemba 04, 2021 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali lililoelekezwa katika Wizara yake linalotaka kufahamu idadi kamili ya mabilionea waliopo nchini.
Aidha amesema kuwa mabilionea 115 kati ya 5,740 wanautajiri wa zaidi ya dola milioni 30 sawa na shilingi bilioni 69.20 za Kitanzania na kwamba wanamiliki zaidi ya 28% ya Utajiri wote wa Mabilionea wanaotoka Tanzania
“Tanzania ina mabilionea 5,740 na wanamiliki jumla ya asilimia 4.2 ya utajiri katika kundi la mabilionea wa Afrika na kati yao mabilionea 115 wana utajiri wa zaidi ya dola milioni 30 na wanamiliki zaidi ya asilimia 28 ya utajiri wote wa mabilionea nchini na wamesajiliwa na TRA,” amesema Dkt. Mwigulu.
Social Plugin