Picha hii ya maktaba haina uhusiano na tukio la Lindi
Dereva wa gari ya abiria mali ya kampuni ya AJ SAFARI linalofanya safari zake kutoka wilayani Liwale Mkoani Lindi kuelekea mkoani Dar es Salaam, amefariki dunia mara baada ya gari hilo kuvamiwa na kundi la nyuki katika eneo la Mbuyuni kata Njinjo wilayani Kilwa mkoani Lindi.
Akithibitisha kupokea majeruhi 22 wa tukio hilo Muuguzi na Mkunga wa kituo cha afya cha Njinjo Albert Filbert amesema walipokea mwili wa dereva huyo aliyejulikana kwa jina la Ally Kalanje.
Wakizungumza na Mashujaa FM, baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo akiwemo kondakta wa gari hiyo Said Chikonda , wameeleza kuwa, tukio hilo limetokea wakati walipokuwa kwenye matengenezo ya gari hilo.
Ghafla kundi la nyuki wakavamia gari na kuzua taharuki kwa abiria takribani 46 waliokuwemo kwenye basi na kuanza kukimbia kutafuta msaada.
Chanzo;Mashujaa Fm
Social Plugin