RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Prof. Wineaster Saria Anderson kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu iliyotolewa leo Novemba 9, 2021 imeeleza kuwa Prof. Anderson anachukua nafasi ya Prof. Eleuther Mwageni ambaye alifariki mwezi Julai, 2021.
Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa, uteuzi huo umeanza Novemba 7, 2021
Social Plugin