Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAIAGIZA TAKUKURU KUWEKA MASANDUKU YA MAONI TAASISI ZOTE ZA SERIKALI

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Mohamed Mchengerwa

Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa maagizo kwa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa nchini[TAKUKURU]kuhakikisha inaweka masanduku ya maoni kuhusu viashiria vya rushwa katika taasisi zote za serikali pamoja na wizara ili kuweza kupokea maoni ya wananchi juu ya viashiria vya rushwa katika taasisi hizo.

Mhe. Mchengerwa ametoa maagizo hayo Novemba 25,2021 jijini Dodoma katika mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU ambao unatoa fursa kwa viongozi wa TAKUKURU kutathimni utendaji wa kazi wa mwaka mzima uliopita kwa mujibu wa sharia ya kuzuia na kupambana na rushwa Namba 11 ya mwaka 2007.

Waziri Mchengerwa amesema viongozi walio wengi hawatambui kuwa nchi ni ya wananchi hivyo TAKUKURU ina nguvu kubwa katika kupambana na viongozi wasio waaminifu.

Hivyo,Waziri Mchengerwa ameiagiza TAKUKURU kuandaa masanduku katika taasisi zote ili kubaini wapokeaji rushwa katika taasisi hizo huku akibainisha kuwa katika mwaka huu ,serikali imetoa kibali cha ajira mpya 350 kwa TAKUKURU.


Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini [TAKUKURU]Kamishna wa polisi , SALUM RASHID HAMDUNI amesema hadi sasa TAKUKURU imeshashinda kesi za rushwa 345 na kushindwa kesi 156 huku ikiokoa Tsh.bilioni 29.3 .

Ikumbukwe kuwa ,mwaka 1971 ilitungwa sheria ya kuzuia Rushwa Na.16 ili kukabili tatizo la rushwa nchini ,baada ya miaka mitatu ,Januari 15,1975 serikali ilianzisha kikosi cha cha kuzuia rushwa chenye dhamana ya kutekeleza sharia Na.16/1971 na kilikuwa chini ya jeshi la polisi na mwaka 1991 sheria ya kuzuia Rushwa Na.16/1971 iliboreshwa ili iendane na wakati na ikaitwa Taasisi ya Kuzuia Rushwa [TAKURU] na wengi walizoea kama PCB ,na ilipofika mwaka 2007 ilibadilishwa kuwa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa [TAKUKURU].

Hivyo mabadiliko haya yaliendana na ongezeko la Wigo wa kushughulikia makossa ya rushwa kutoka makosa 4 na kuwa makossa 24 chini ya sharia ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007 inayotumika hadi sasa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com