Mkandarasi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA),kutoka Kampuni ya M/s Central Electrical ameanza kazi ya kutawanya nguzo za umeme katika Tarafa ya Mungaa jimbo la Singida Mashariki.
Akizungumza baada ya kukagua uanzaji wa kazi ya usambazaji kwenye maeneo ya Kitongoji Cha Sie Kijiji Cha Mungaa,Katibu wa mbunge wa jimbo hilo Nicodemus Mwaya ameishukuru serikali kwa kutimiza ahadi yake.
"Tunaishukuru serikali kwa kusikia kilio Cha mbunge wetu Miraji Mtaturu,haya ni matunda yake,mara kadhaa amekuwa akiikumbusha serikali kupitia maswali anayouliza na michango anayoitoa bungeni,lakini pia amefuatilia wizarani Ili kuweka msukumo wa utekelezaji,tunamshukuru sana,
"Niahidi tu katika kipindi hiki ambacho Mbunge wetu anatekeleza majukumu mengine ya kibunge nje ya jimbo, mimi Katibu wake na viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya,na diwani tutakuwa tunapita mara kwa mara Ili kuona namna kazi inavyoendelea,lengo letu ni kuhakikisha dhamira ya serikali ya kufikisha umeme kwenye kila Kijiji inafikiwa,"aliongeza.
Singida Mashariki #MaendeleoKipaumbeleChetu#
Social Plugin