****************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Klabu ya Simba Sc yafanikiwa kuondoka na alama tatu muhimu kwenye mchezo dhidi ya Namungo ambapo wameshinda 1-0 katika dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake, kulishuhudiwa na kadi nyekundu kwa mchezaji wa Namungo Fc kiungo Abdulaziz Makame baada ya kumchezea rafu mbaya Shomari Kapombe.
Simba ilifanya mabadiliko ya wachezaji kadhaa ambao walichangia kwa kiasi kikubwa kupata matokeo mazuri.
Meddie kagere ndiye aliyeokoa jahazi mara baada ya kufunga kwa kichwa akipokea krosi kutoka kwa beki Mohamed Husein dakika ya 95 ya mchezo.
Social Plugin