Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa mwaka wa utamaduni wa usalama wa usafiri wa anga uliofanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa akikaguliwa kama sehemu ya Uzinduzi wa mwaka wa utamaduni wa usalama wa usafiri wa anga uliofanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa akikaguliwa kama sehemu ya Uzinduzi wa mwaka wa utamaduni wa usalama wa usafiri wa anga uliofanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Profesa Makame akifuatiwa na baadhi ya watendaji wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kukaguliwa ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa mwaka wa utamaduni wa usalama wa usafiri wa anga
Waziri wa Ujenzi na uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akizungumza katika uzinduzi wa mwaka wa Utamaduni wa Usalama wa Usafiri wa Anga (YEAR OF SECURITY CULTURE – 2021 ) iliyofanyika Makao makuu ya Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi Mamlaka ya Usafiri wa anga Tanzania (TCAA) Prof. Longinus Rutasitara akizungumza katika uzinduzi wa mwaka wa Utamaduni wa Usalama wa Usafiri wa Anga (YEAR OF SECURITY CULTURE – 2021 ) iliyofanyika Makao makuu ya Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) jijini Dar es Salaam. Mkururgenzi Mkuu – Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari akizungumza katika uzinduzi wa mwaka wa Utamaduni wa Usalama wa Usafiri wa Anga (YEAR OF SECURITY CULTURE – 2021 ) iliyofanyika Makao makuu ya Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa Usalama wa Usafiri wa Anga
Wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi huo.
Waziri wa Ujenzi na uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amewaagiza wakuu wa Taasisi za usafiri wa anga nchini kuhakikisha kila mtumishi aliyepo au anayefanya kazi kwenye viwanja vya ndege, Mashirika ya ndege na watoa huduma wengine kutii na kufuata taratibu za kiusalama zilizopo kwa mujibu wa miongozo ya kitaifa na kimataifa.
Rai hiyo ameitoa mapema leo wakati akihutubia katika uzinduzi wa mwaka wa Utamaduni wa Usalama wa Usafiri wa Anga (YEAR OF SECURITY CULTURE – 2021) iliyofanyika Makao makuu ya Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) jijini Dar es Salaam.
Prof. Mbarawa amesema kuwa suala la usalama katika viwanja vya ndege ni muhimu kuzingatiwa kwani bila kutiliwa mkazo linaweza kuleta maafa makubwa.
“Viongozi naomba mtilie mkazo swala la ukaguzi halina msamaha isipokuwa kwa viongozi wakuu wa nchi wanaomtambulika kisheria. Kukataa au kukaidi kukaguliwa ni kukiuka sheria za nchi na za Kimataifa,” Amesema Prof. Mbarawa.
Amesema kuwa usafiri wa anga ni salama kuliko njia nyingine zote za usafiri duniani. Usalama huu wa usafiri wa anga ni mafanikio makubwa ambayo hayatokei yenyewe, bali kwa jitihada mbali mbali zinazofanywa na wataalam wa usafiri wa anga hapa nchini na duniani kwa ujumla kwa kushirikiana pamoja kuweka mifumo na kanuni za uendeshaji na usimamizi wa shughuli zote za usafiri wa anga.
“Pamoja na jitihada hizi, ni wazi kwamba suala la usalama wa anga (Aviation Security) limekua na changamoto duniani kote zitokanazo na uwepo wa matishio au matendo ya kigaidi kwa kipindi fulani na wakati mwingine kurudi katika hali ya kawaida au kuonekana kuwa katika hali ya kawaida kinyume na uhalisia. Changamoto hii imepelekea madhara kadhaa duniani ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha ya wasafiri wa ndege na hata wasiosafiri, uharibifu wa mali na miundombinu, kuzorota kwa shughuli za utalii na biashara duniani kutokana na hofu ya vitendo vya kigaidi dhidi ya usafiri wa anga. Kutokana na hali hii, mbinu za kukabiliana na changamoto hizi zinapaswa kuwa endelevu na shirikishi ili ziweze kuwa na tija,” Amesema.
Amesema mwaka 2021 ni mwaka muhimu katika historia ya usalama wa usafiri wa anga kwani ndio kumbukizi ya miaka 20 ya tukio la utekaji nyara wa ndege 4 za abiria ambazo hatimae zilitumika kama silaha kwa magaidi kutungulia majengo mawili ya kibiashara na jengo la makao makuu ya wizara ya ulinzi nchini Marekani. Tukio hili maarufu kama 9/11 ,(yaani 11 Septemba 2001) lilipelekea vifo vya maelfu ya watu waliokuwa ndani ya ndege hizo pamoja na majengo yaliyotunguliwa na ndege hizo. Mbali na vifo hivyo, zilijitokeza athari nyingi sana kiuchumi na hata kijamii duniani kote mpaka sasa. Hali hii inatukumbusha kwamba, Usalama ni wajibu wa kila mtu, kila nchi na hata taasisi moja moja, kwani bila kujali tukio limetokea wapi na nani amesababisha, madhara ya tukio hilo yatatufikia sote.
Kwa upande wake Mkururgenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari ametilia msisitizo na kuahidi kulisimamia suala a ukaguzi katika viwanja vya ndege na kutoa wito kwa watendaji wengine kutona kero pindi wanapolazimika kukaguiwa.