Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera hivi karibuni akiwa mgeni rasmi amekabidhi Trekta ndogo (Powertillers) aina ya Kubota 241 zenye thamani ya Tshs. 2.6 Billion, vifaa hivyo vimetolewa na kampuni ya Agricom Africa Kwa udhamini wa mkopo kupitia CRDB Bank kwa wakulima wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Mtendaji Mkuu wa Agricom Africa Ltd Bw. Alex Duffar akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya matrekta yaliyotolewa na Agricom Africa ltd kupitia udhamini wa mkopo wa CRDB Bank
Mwakilishi wa Meneja wa kanda WA Benki ya CRDB nyanda za juu kusini akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya matrekta yaliyotolewa na Agricom Africa ltd kupitia udhamini wa mkopo wa CRDB Bank Igurusi mbeya
Picha ya pamoja Kati ya mkuu wa mkoa wa Mbeya na wakulima waliokabidhiwa trekta ndogo aina ya Kubota Powertillers
Mkuu wa mkoa wa Mbeya,mwakilishi wa Meneja wa kanda WA Benki ya CRDB na Mtendaji Mkuu wa AGRICOM AFRICA LTD wakiwa na funguo kama ishara ya makabidhiano ya matrekta yaliyotolewa na Agricom Africa ltd kupitia udhamini wa mkopo wa CRDB Bank.
Social Plugin