Mkazi wa Kijiji cha Itolwa wilayani Chemba mkoani Dodoma, Juma Juma (34) amefariki dunia baada ya kuukata uume wake kutokana na kile kinachoelezwa kuwa alipoteza nguvu za kiume.
Inaelezwa kuwa Juma amefikia uamuzi huo wa kuukata uume wake baada ya kupata ajali na kuteguka kiuno na kusababisha asiwe rijali.
Akizungumzia juu ya tukio hilo Mwenyekiti wa kijiji hicho, Daudi Ally amesema leo Jumatatu Novemba 22, 2021 Juma amefariki baada ya kupungukiwa maji pamoja na damu.
Akizungumzia tukio hilo, mjomba wa Juma, Yasini Nkusa amesema tukio hilo la Juma kujikata uume lilitokea Ijumaa nyumbani kwake Kijiji cha Itolwa ambapo alitumia wembe kukata uume wake.
Juma ambaye ameacha mke na watoto watatu alipata ajali ya gari wiki mbili zilizopita.
Chanzo- Mwananchi
Social Plugin