Baadhi ya Maafisa wa WMA wakihakiki mawe ya mizani ya kupima uzito wa magari makubwa wakati wa uhakiki wa Vipimo ukihusisha maafisa vipimo nchi nzima leo katika Makao Makuu ya WMA Jijini Dar es Salaam Baadhi ya Maafisa wa Vipimo wakihakiki mawe ya mizani wakati wa uhakiki wa Vipimo ukihusisha maafisa vipimo nchi nzima leo katika Makao Makuu ya WMA Jijini Dar es Salaam Baadhi ya Maafisa wa Vipimo WMA wakihakiki mawe ya mizani wakati wa uhakiki wa Vipimo ukihusisha maafisa vipimo nchi nzima leo katika Makao Makuu ya WMA Jijini Dar es SalaamAfisa Vipimo akihakiki mawe ya mizani wakati wa uhakiki wa Vipimo ukihusisha maafisa vipimo nchi nzima leo katika Makao Makuu ya WMA Jijini Dar es Salaam
Afisa Vipimo akihakiki mawe ya mizani wakati wa uhakiki wa Vipimo ukihusisha maafisa vipimo nchi nzima leo katika Makao Makuu ya WMA Jijini Dar es Salaam
Mawe ya mizani ikiwa tayari kwa kufanyiwa uhakiki na kututumika katika vipimo sahihi leo wakati wa uhakiki wa Vipimo ukihusisha maafisa vipimo nchi nzima leo katika Makao Makuu ya WMA Jijini Dar es Salaam Baadhi ya mizani ikiwa tayari kwa kufanyiwa uhakiki na kututumika katika vipimo sahihi leo wakati wa uhakiki wa Vipimo ukihusisha maafisa vipimo nchi nzima leo katika Makao Makuu ya WMA Jijini Dar es Salaam
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Wakala wa vipimo nchini (WMA ),imewataka wananchi kutoa taarifa au malalamiko ya uwepo wowote wa changamoto zinazotokana na masuala ya vipimo katika maeneo wanayopata huduma.
Akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa uhakiki wa Vipimo ukihusisha maafisa vipimo nchi nzima ,Kaimu Mkurugenzi Mkuu WMA Bi.Stella Kahwa, amesema kuwa wako kwenye uhakiki ambao vipimo hivyo vitatumika na Maafisa vipimo katika kuweka sawa ulinganisho wa vipimo nchi nzima.
Amesema kuwa ni wakati sasa wananchi kuwasiliana kwa namba zao pindi inapojitokeza changamoto zozote za masuala ya vipimo.
"Vipimo vinavyotumika huwa vinakaguliwa mara moja kwa mwaka au pale ikionesha kuna changamoto ambapo vinalinganishwa na vipimo vya kimataifa na vinalingana kwa kila nchi Duniani". Amesema
Kwa upande wake Afisa Vipimo Mwandamizi kutoka Mkoa wa Mtwara Bw.Shomari Shomari amesema kuwa umuhimu wa kupima kwa pamoja ni kuhakikisha vipimo hivyo vinakuwa sahihi kwa mikoa yote kutokana vifaa vya vipimo hupungua usahihi mwaka kila mwaka.
Naye Afisa Vipimo Mwandamizi Kutoka Jijini Mwanza Bw.Barisico Kapesa, amewahakikishia wananchi kuwa baada ya kufanya uhakiki huo vipimo vyote vitakuwa na usahihi kwa nchi nzima kwa kimataifa.