WANANCHI WATAKIWA KULINDA MIUNDO MBINU YA TANESCO



.........................................................


Wananchi wametakiwa kulinda miundo mbinu ya Tanesco dhidi ya watu wasiowaadilifu wanaoiba miundo mbinu hiyo huku wananchi wenye tabia ya kuchoma nguzo wametakiwa kuacha tabia hiyo mara moja .


Akitoa elimu kwa wananchi juu ya masuala ya ulinzi wa miundo mbinu ya Tanesco mkoani Morogoro katika vijiji vyote vilivopo mkoani Afisa kutoka kitengo cha masoko makao makuu Tanesco Bi Jennifer Mgendi amewasisitiza wananchi kulinda miundombinu kwa kuwataka kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake.


Aidha Bi. Mgendi ameendelea kutoa ushauri kwa wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya matapeli (VISHOKA) wanao watapeli na kujifanya wanatokea TANESCO kwa kuwadhulumu fedha .


“Fedha zote za serikali hulipwa kwa kupitia control namba pekee mtu yoyote asije akawadanganya mkampa fedha bila kutumia control namba watu wanaibuka ili kuwaibia nyie wananchi msiojua hivyo kila mmoja asikubaili kulipa fedha yoyote na kwa mtu yoyote bila kutumia control namba”amesema Bi.Mgendi.


Hata hivyo wananchi wametakiwa kuchangamkia fursa ya umeme kwa kuwanufaisha katika kuwaingizia kipato lengo ikiwa ni kuwainua kiuchumi .


“Umeme ni kitu muhimu sana kwa maendeleo katika maisha kukua kwa sayansi na teknolojia umeme huu umetusaidia kurahisisha maisha na ndio maana tunahakikisha kila mwananchi anapata umeme bila kujali hali ya maisha aliyonayo.”Amesema Bi. Mgendi.


Amesema wananchi wametakiwa kutokufanya shughuli za kijamii chini ya miundo mbinu kama laini au transfoma kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha afya zao .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post