Watatu wafariki kwa kufukiwa na kifusi Sikonge


Na Lucas Raphael,Tabora

Watu watatu wamefariki dunia wakiwemo watoto wawili na  mwanafunzi mmoja  wa shule ya msingi majengo wilaya ya sikonge mkoani Tabora baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba molamu..

Kamanda wa polisi mkoani Tabora akizungumza na waandishi wa habari jana Richard Abwao alisema kwamba tukio hilo lilitokea katika kitongoji cha Usenga kijiji cha misheni kata ya misheni wilaya ya sikonge mkoani hapa

Alisema kwamba mnamo Novemba 16 mwaka huu majira ya saa 12 na 30 jioni  katika shimo lililokuwa limechibwa na wachina wanaojenga barabara wilayani humo.

Alisema kwamba chanzo ni kuporomoka kwa kifusi /udogo na kuwaangukia marehemu wakati wakiwa chini wakichimba molamu hiyo.

Kamanda huyo wa polisi aliwataja walifariki kuwani mwanafanzi Rashid Hamis (9) Sadiki Ramadhani (9) na  Bakari Shabani (21).

Aidha aliwataka wananchi wote wa mkoa wa Tabora kuchukua tahadhari katika maeneo ya ujenzi ambayo kuna mashimo makubwa ili kuepukana na madhara hasa tunavyoelekea katika kipindi masika.

mwisho



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post