WATU 115 walifariki katika mlipuko wa tenki la mafuta siku ya Ijumaa, nchini Sierra Leone wanazikwa kwa pamoja katika mji mkuu wa Freetown. Wengi waliungua sana hata ikawa vigumu kuwatambua.
Mamlaka imetoa wito wa watu kujitolea damu kwa haraka ili kuweztibu wahanga walioungua na moto ambao ni zaidi ya 100 wamelazwa hospitalini. Maofisa wanasema wasambazaji wa damu wanaweza kuishiwa ndani ya saa 72.
Mazishi hayo yamefanyika katika eneo ambalo watu wapatao 1000 walizikwa mwaka 2017 baada ya kuuawa kutokana na mmomonyyoko wa udongo, anasema mwandishi wa nchini humo Umaru Fofana.
Msemaji wa waziri wa afya amethibitisha kuwa idadi ya vifo vilivyotokea katika ajali ya Ijumaa ni 115. Rais Julius Maada Bio ametangaza siku tatu za maombolezo kitaifa na bendera kupeperushwa nusu mlingoti kufuatia janga lililotokea Ijumaa.