WATUMISHI WIZARA YA AFYA WANAOUZA DAMU WAPEWA ONYO


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amewaonya watumishi wanaofanya biashara ya kuuza damu kinyume cha sheria za nchi na kwamba hata sita kuwawajibisha watakao bainika wanaowashurutisha ndugu wa mgonjwa kutoa damu kabla ya kumhudumia mgonjwa hali inayosababisha kuhamasisha vitendo vya rushwa na kuhatarisha maisha ya wagonjwa.

Dkt Gwajima amefikoa hatua hiyo wakati akiongoza tamasha la uchangiaji damu kutoka makundi ya vijana wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi sambamba na utoaji wa Chanjo za UVIKO 19 ambapo vijana hao wamefanya matembezi ya hiyari wakihamasisha jamii umuhimu wa kujikinga na magonjwa hatarishi.

“Mpango wa Taifa wa Damu Salama hutoa damu bila malipo kwa hospitali zote hivyo wagonjwa wote wanatakiwa kupata tiba ya damu bila malipo yoyote aidha wananchi wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa serikali kuwafichua wale wote watakao bainika wanaouza damu salama kwenye vituo vya afya ili wawajibishwe kisheria” Amesema Dkt. Gwajima.

Aidha Dkt Gwajima ametoa siku 30 kwa taasisi ya kuratibu mpango wa Taifa wa Damu Salama kushirikisha wadau wengine wote wakiwemo Chama cha Msalaba Mwekundu kuhakikisha kinatafuta namna ya kuratibu upatikanaji wa damu salama zaidi ya chupa 550,000 zitakazo tosheleza mahitaji ya hospitali na vituo vya afya hapa nchini ili kunusuru vifo vya wagonjwa vinavyosababishwa na upungufu wa damu.

Amesema kuwa maisha ya mwanadamu yanategemea damu salama ambapo kundi kubwa la watoto chini ya miaka mitano wanahitaji damu kwa asilimia 50 ikifatiwa na kundi la mama wajawazito aslimia 30, ajali mbalimbali ikiwemo waendesha pikipiki bodaboda asilimia 15 na asilimia 5 hupelekwa kwa wagonjwa wa saratani na upasuaji mkubwa wa moyo.

Dkt Gwajima amesema kuwa shirika la afya Duniani linapendekeza kuwa ili nchi iweze kukusanya damu ya kutosha inapashwa kukusanya chupa za damu kutoka kwa asilimia moja ya idadi ya watu katika taifa ambapo hapa nchini inatakiwa kukusanya damu chupa kumi kati ya watu 1000,

Kwa sasa Mpango wa Taifa wa Damu umeweka malengo ya kukusanya damu salama chupa 550,000 ambapo vijana wamekuwa mstari wa mbele kujitolea kutoa damu inayokusanywa hapa nchini kwa asilimia 80 ila kutokana na hamasa ndogo ya wananchi zinakusanywa chupa 312,907 sawa na chupa sita kwa watu 1000.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratan Ocean Road Dkt.Julius Mwaiselage amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan Kwa kuipatia fedha taasisi ya Ocean Road Kiasi cha shilingi Bilioni 5.4 kwa ajili ya kuboreha huduma ya afya ikiwemo kununua mashine ya MRI na kuanzisha kitengo cha ICU hali itakayopunguza kusafirisha wagonjwa kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa James Fondation James Yusta ameimba serikali kuanzisha Mfumo wa elimu ya malezi bora katika shule za msingi,sekondari na vyuo ili kuandaa watoto kuwa wazazi na walezi bora katika familia kwa lengo la kutokomeza wimbi la watoto wanaoishi katika mazingira

Tamasha hilo lilme andaliwa na kijana aliyetupwa vichakani na kutelekezwa na wazazi wake ambaye ameishi mazingira magumu na hatarishi aitwaye James Fondation ambaye kwa kushirikiana na serikali na asasi zingine za kirai kwa pamoja wanahamasisha jamii kuchangia damu salama kwa manufaa ya Taifa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post