Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda(wa pili kushoto) akimkabidhi pikipiki afisa kilimo wilaya ya Bariadi Wilbard Siogopi, kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi Lupakisyo Kapange.
Na Costantine Mathias, Simiyu.
WAZIRI wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda amekabidhi pikipiki 86 kwa Maafisa ugani wa mkoa wa Simiyu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha kuwa zao la pamba linasimamiwa kikamilifu katika mkoa huo katika msimu huu wa kilimo wa mwaka 2021/2022.
Pikipiki hizo ni sehemu ya pikipiki 250 zilizonunuliwa na Bodi ya Pamba Nchini (TCB) kwa maafisa ugani wa mikoa 17 inayolima zao hilo na zimegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 525.
Akikabidhi pikipiki hizo jana kwa Wakuu wa wilaya za Maswa, Meatu, Busegà , Bariadi na Itilima zilizoko katika mkoa huo amesema kuwa bajeti ndogo inayotengwa kwenye halmashauri za wilaya kwa idara ya kilimo,umwagiliaji na ushirika ni ndogo na hivyo kuwafanya washindwe kufanya majukumu yao kwa ufanisi.
Amesema idara hiyo imekuwa ikitupiwa lawama hasa kwa Maafisa Ugani kwa kushindwa kusimamia kilimo wakati huo kwa kutowafikia wakulima hasa maeneo ya vijiji kwa kutokuwa na vitendea kazi kama vile pikipiki.
"Hatuwezi kuongeza tija kwenye kilimo kama hatutaweza kuwathamini Maafisa Ugani tutaendelea kuwalaumu kwa mfano Mkuu wa idara ya kilimo katika halmshaurk hana gari je atawafikiaje wakulima huko vijiji lakini idara kama Elimu na idara ya Afya zenyewe zina magari mazuri kwa msingi huo ni lazima tuwathamini kabla ya kuwalaumu,"amesema.
Amesema idara ya kilimo katika mikoa inayolima zao la pamba ndiyo imekuwa ikiingiza mapato mengi katika halmashauri za wilaya lakiñi bado mkuu wa idara hana gari la kufanyia kazi.
"Ili kuonyesha kuwa hawa wakuu wa idara za kilimo hawapewi kipaumbele katika masuala ya vitendea kazi mfano wilaya ya Meatu mkoani hapa ilikusanya kiasi cha Sh Bilioni1.2 za ushuru wa pamba katika msimu uliopita lakini Mkuu wa idara ya kilimo hana gari bali ana pikipiki tu hiyo ndiyo awatembelee wakulima wote katika wilaya hiyo hii haiwezekani,"amesema.
Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda (wa pili kushoto) akimkabidhi pikipiki afisa kilimo wilaya ya Maswa Peter Bujimu, kulia ni mkuu wa wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge.
Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda(wa pili kushoto) akimkabidhi pikipiki afisa kilimo wilaya ya Bariadi Wilbard Siogopi, kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi Lupakisyo Kapange.
Social Plugin