Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ameruhusu kusafirisha makontena 187 ya Vinia kwenda nchi za nje yaliyokuwa yamekwama bandarini baada ya kutoa tamko la kuzuia usafirshaji malighafi za mazao ya misitu kwenda nchi za nje ikiwemo vinia
Vinia ni malighafi iliyochakatwa nusu kutoka kwenye gogo ambalo Wawekezaji wengi husafirisha nje ya nchi kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali hususan mbao laini (plywood) ambazo hurejeshwa tena nchini kuuzwa kwa bei ya juu
Plywood ndiyo inayotumika katika shughuli za ujenzi wa maghorofa na kutenganisha vyumba katika ofisi, Licha ya kuruhusu usafirishaji wa makontena hayo 187 yaliyokuwa na vinia, Dkt. Ndumbaro ameendelea kushikilia msimamo wake wa kutoruhusu uvunaji na biashara ya gundi ndani na nje ya nchi mpaka pale watafiti watakapotoa hasara na faida yake.
Hatua hiyo inakuja kufuatia ombi la Wafanyabishara wa mazao ya misitu wakimtaka aongeze muda wa kusafirisha mazao ya misitu kwenda nchi za nje baada ya kupigwa marufuku kuanzia Novemba 15 mwaka huu.akiwa mkoani Iringa
Waziri Dkt. Ndumbaro ametoa ruhusa hiyo leo wakati alipokuwa akizungumza na k Wafanyabishara wa mazao ya misitu katika mkutano ulioitishwa na Wafanyabiashara hao Jijini Dar es Salaam kupitia Baraza la Taifa la Wafanyabishara (TNBC) wakiomba kuongezewa muda wa kusafirisha mazao hayo.
Akifafanua ruhusa hiyo, Dkt. Ndumbaro amesema ruhusa hiyo inahusu makontena 187 tu ambayo yapo tayari yameshafika bandarini na sio kwa makontena ambayo hayako bandarini
''Naomba nieleweke vizuri ruhusa hii ya kusafirisha vinia itahusu makotena 187 tu ambayo nyaraka zake tayari zilishawasilishwa kwenye vyombo vya kiserikali'' amesisitiza Dkt, Ndumbaro
Katika hatua nyingine, Serikali imewaongezea muda Wafanyabiashara wa mazao ya misitu nchini kusafirisha vinia kuanzia leo hadi tarehe 30 Juni 2022 kwa vigezo na masharti kuzingatiwa
Akitaja masharti hayo Dkt. Ndumbaro amesema Wafanyabiashara watakaoruhusiwa kusafirisha vinia kwa kwa kipindi hicho tajwa watatakiwa kuwasilisha mpango kazi wa kuleta mashine ya kuchakata vinia hadi hatua za mwisho pamoja na kuwasilisha taarifa za kodi na malipo mengine ya serikali
Mbali na Mashart hayo, Dkt. Ndumbaro amesema wafanyabiashara hao ili waweze kuruhusiwa kusafirisha mazao hayo watatakiwa kuwasilisha taarifa za haki za Wafanyakazi katika viwanda vyao pamoja na gharama halisi za mzigo huo
Hata hivyo, Dkt. Ndumbaro ametoa onyo kwa Mfanyabishara yeyote atakayetoa taarifa za uongo na akathibitika hatapewa ruhusa ya kusafirisha vinia hiyo huku akisisitiza kuwa katika kipindi hicho cha mpito yeye mwenyewe Waziri ndiye aatakayehusika na kutoka vibali kwa Wafanyabishara vya kuruhusu kusafirisha vinia kwenda nchi za nje
Kwa upande wake Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Taifa la Wafanyabaishara (TNBC) Ben Sulus amemshukuru Waziri kwa kukubali ombi la Wafanyabishara hao la kuongezewa muda huku akisisitiza kuwa ni muda muafaka sasa kwa Wafanyabishara hao kuungana kwa pamoja kuleta mashine ambazo zitachakata vinia hozo hadi hatua za mwisho ili kutoa ajira kwa wananchi wanaozunguka misitu hiyo.
Naye Mfanyabishara wa Kiwanda cha Vinia cha Yu lin , Ben Makombe amesema Wizara ina lengo jema lakini wanaomba kuongezwa muda takriban mika mitatu ili waweze kukusanya fedha kwa ajili ya kununua mashine ambazo zitaweza kuchakata vinia hizo hadi hatua za mwisho
Amefafanu kuwa mashine hizo zinauzwa dola 8,000 hivyo zinahitaji Wafanyabaishara wenye mitaji mikubwa hivyo endapo watapewa muda wataweza kuzinunua.
Social Plugin