Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Wakati naingia OR-TAMISEMI nilikuta umeanza mchakato wa kuifuta Idara ya Mipango miji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, sasa tunairudisha na tunaiita Idara ya uendelezaji wa miji na vijiji na kazi yake kubwa itakuwa ni kuhakikisha miji yetu inapangwa, miji yetu inapimwa, miji yetu inaendelezwa.”
Hayo yamesema na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizungumza kwenye semina ya Wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania bara iliyolenga kuwapa uelewa wa namna ya kutekeleza mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi.
Mhe. Ummy aliongeza: “tumeshabainisha miji inayochipukia kama 2,310, katika mikoa yetu na tumebainisha meneo ambayo yanachipukia badala ya kusubiri mpaka tuje tupambane kama tunavyopambana na wamachinga sasa hivi, hatutaacha watu wajenge holela holela na kupitia Idara hii ya Uendelezaji Miji na Vijiji watakua na jukumu kubwa la kusimamia ukuaji wa miji hiyo inayochipukia.
Alizungumzia kuhusu Anwani za Makazi na Postokodi amesema Miji yetu inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa uhalifu na ugumu wa kufika katika maeneo fulani utakuta unamwambia mtu ukifika daraja la kwanza, la pili la tatu kata kona kulia, kona kushoto ni ngumu sana lakini mfumo huu wa anwani za makazi utasaidia.
WAZIRI amesema mfumo huu wa anwani za makazi na postikodi utasaidia katika Mpango wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI ya kuiendeleza na kuipanga miji hususani miji inayochipukia
Wakati huo huo Mhe. Ummy amesema Idara ya Usafishaji na Mazingira katika Halmashauri itasimamiwa na Idara ya Uendelezaji Miji kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI.