Ruvu Shooting ilianza kupata bao dakika ya 8 ya mchezo kupitia kwa nyota wao Rashid Juma.
Yanga iliwachukua dakika 32 kusawazisha bao likifungwa na Feisal Salumu "Fei toto" kwa shuti kali ambalo lilimshida kipa wa Ruvu Shooting Makaka na kuingia nyavuni.
Kipindi cha pili kilianza huku Yanga ikiendelea kutawala mchezo mara baada ya Ruvu Shooting kucheza pungufu baada ya nahodha wao Santos kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu mbaya mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele.
Iliwachukua dakika 2 kipindi cha pili kupata bao mara baada ya mchezaji wa Ruvu Shooting kunawa mpira ndabi ya box na kuamuliwa penati ambayo ilipigwa na Djuma Shaban.
Bao la tatu la Yanga lilifungwa na Mukoko Tonombe mara baada ya kupewa basi tamu na Farid Mussa na kuachia shuti kali ambalo lilimshinda kipa na kuingia wavuni.
Yanga inaendelea kuongoza ligi kwa kucheza mechi tano na kujikusanyia pointi 15 huku akiruhusu bao moja tu katika michezo hiyo.
Social Plugin