MTU mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Joseph, Mkazi wa Makambako mkoani Iringa amefariki dunia huku wengine wawili wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mawili yaliyogongana uso kwa uso ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.
Ajali hiyo imetokea jana Ijumaa, Desemba 10, 2021 na kuhusisha gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T 948 DGQ lilikuwa likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Njombe likiwa na watu wawili (dereva na kondakta) ambaye amepoteza maisha.
Fuso hilo lilikuwa na mzigo wa juisi na tambi za huku gari jingine ambalo ni Lori la mizigo lililokuwa linatokea nchini Zambia likiwa na namba za usajili T 299 CXU likiwa na mzigo wa madini aina ya Copper.
Ofisa Uhifadhi wa Daraja la Kwanza, Dr. Isaya Kiwale wa Kitengo cha Sayansi Uhifadhi amethibitidha kutokea kwa ajali hiyo ndani ya hifadhi hiyo.
Social Plugin