Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WALIOFARIKI KWENYE BASI LILILOSOMBWA NA MAJI WAFIKIA 33...BASI LATOLEWA


Shughuli za uokoaji ziliendelea siku ya Jumapili kufuatia ajali mbaya iliyotokea Jumamosi katika mto wa Enziu, kaunti ya Kitui nchini Kenya huku basi lililokuwa limezama likitolewa ndani ya maji. Basi hilo la shule ya upili ya St Joseph Seminary ambalo lilikuwa limeharibika lilitolewa mwendo wa jioni.

MiIli saba zaidi ilipatikana ikiwa imekwama ndani ya basi hilo na kufikisha idadi ya walioangamia kuwa 33. Hapo awali asubuhi ya Jumapili wakati shughuli za uokoaji zilirejea kwa siku ya pili miili miwili zaidi ilitolewa.

Kufikia kusimamishwa kwa shughuli ya uokoaji jioni ya Jumamosi, watu 24 walithibitishwa kufariki huku wengine 12 wakiokolewa. Basi hilo lilitolewa na cranes mbili za NYS na trekta ya kaunti ya Kilifi. Gavana wa Kitui Charity Ngilu alisema msako zaidi ungeendelea siku ya Jumatatu kuhakikisha kwamba hakuna mili mingine iliyokwama ndani ya mto huo.
Alasiri ya Jumamosi basi lililokuwa limebeba abiria zaidi ya 30 waliokuwa wanaenda kuhudhuria harusi liliwezwa na mikondo ya maji yenye nguvu, likapinduka na kuzama ndani ya mto wa Enziu wakati lilijaribu kuvuka daraja lililokuwa limefurika maji.


Abiria waliokuwa ndani ya basi hilo la shule ya Sekondari ya Mwingi Seminary wanaripotiwa kuwa waumini kutoka kanisa ya katoliki ya Mwingi ikiwemo watoto. Kati ya watu 24 ambao mili yao ilipatikana siku ya Jumamosi, 22 walikuwa waumini katika kanisa la St. James Good Shepherd Catholic Church.

Ujumbe wa mawasiliano uliotumwa kwa wanachama wa kanisa hilo ambao umeonwa na Radio Jambo unasema wahasiriwa walikuwa wanaelekea upande wa Nuu kuhudhuria harusi ya ndugu ya Padre Benson Kityambu wa kanisa la katoliki la Mwingi.


Padre Kityambu anaripotiwa kupoteza wapwa wake 11 katika ajali hiyo iliyotokea mwendo wa saa saba alasiri. Ndugu wawili wa kidini ambao walikuwa wanafanya kazi katika seminari pia walipoteza maisha yao kwenye ajali hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com