Mkuu wa wilaya Ilala, Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ndwata Ludigija (kulia) akifurahia na mshindi wa milioni 10 wa Biko, Mikidadi Kaimu Ngoo alipomtembelea ofisini kwake kumkabidhi hundi yake ya ushindi wa Biko. Picha na Mpigapicha Wetu.
Balozi wa Biko Kajala Masanja akipiga picha sambamba na kumkabidhi hundi yake mshindi wa Biko Mikidadi Kaimu Ngoo aliyeshinda Sh Milioni 10 za Bahati nasibu ya Biko maarufu kama Buku Nibukue.
Mkuu wa wilaya Ilala, Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ndwata Ludigija (kulia), akiwa na mshindi wa sh milioni 10, Mikidadi Kaimu Ngoo mwenye maskani yake Chanika, wilayani Ilala, mkoani Dar es Salaam katikati. Kushoto ni Balozi wa Biko Kajala Masanja alipoenda kuungana na DC Ng'wilabuzu Ndwata Ludigija kumkabidhi mshindi huyo hundi yake ya ushindi wa mamilioni ya Biko.
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKUU wa wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ndwata Ludigija, amechagiza utolewaji wa zawadi za mbuzi za sikukuu ya Christmass na Mwaka mpya zinazotolewa kwa wingi katika ushindi wa papo kwa hapo wa Bahati nasibu ya Biko, akisema zitapunguza makali ya maisha kwa Watanzania watakaofanikiwa kushinda kwenye droo hizo.
Mheshimiwa Ludigija aliyasema hayo wakati wa makabidhiano ya hundi ya sh Milioni 10 kwa Mikidadi Kaimu Ngoo wa Chanika, wilayani Ilala, mkoani Dar es Salaam, aliyeshinda kwenye droo ya Jumapili na kuwa miongoni mwa Watanzania wengi wanaobukua mamilioni ya Biko, ambapo katika droo za papo kwa hapo, sh laki mbili mbili zitamwagika kama sehemu ya ununuaji wa mbuzi za sikukuu za mwisho wa mwaka.
Mchezo wa biko unachezwa live mtandaoni kwa kuingia www.biko.co.tz bila kusahau wale wanaotumia njia ya kawaida kwa kucheza kwa namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu 2456 au neno biko, huku kianzio cha kucheza kikiwa sh 1000 na kuendelea.
Biko ni mchezo wa kubahatisha unaoongoza kutoa fedha nyingi kwa Watanzania, ambapo zwadi za papo kwa hapo zinatoka kila sekunde moja kuanzia sh 2500 hadi milioni 5 papo hapo bila kusahau kutoa zawadi ya hadi sh milioni 40 kila Jumapili ambapo mbali na kucheza kwa namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu 2456, pia watu wanaweza kucheza live kwa kuingia www.biko.co.tz.