CCM KUWACHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU WATAKAOBAINIKA KUANZA KAMPENI ZA UCHAGUZI

Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akiongea wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi Taifa Jijini Dodoma.

Na Dotto Kwilasa, Malunde 1 Blog, DODOMA.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakitasita kuwachukulia hatua za kinidhamu  wale ambao watabainika  kufanya kampeni za uchaguzi mkuu wa chama hicho pamoja na kutoa  na kupokea rushwa huku kikidai kuwa kitendo hicho  ni kinyume cha maadili ya chama hicho.


Hayo yameelezwa leo na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi Taifa Jijini Dodoma.

Kanali Lubinga amesema mwaka 2022 ni mwaka wa uchaguzi wa ndani ya chama na jumuiya zake ambapo amedai uchaguzi maana yake ni mfumo wa kijamii ya kistaarabu kupata uongozi,kuendesha jumuiya na kwa lugha ya kisiasa ni sehemu ya kidemokrasia.

Katibu huyo wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa alisema chama kina imani uchaguzi huo utaendeshwa kwa ustaarabu na kanuni za Chama na Jumuiya lakini akadai kampeni zake bado muda na ukifika wataarifiwa  na wote ni lazima wazifuate.

Kwa upande wake,Katibu wa Organization CCM Taifa, ambaye ni Mlezi wa Jumuiya za chama hicho,Dk. Modeline Castica amewashukuru viongozi mbalimbali wa Jumuiya hiyo kwa kusimamia mambo mbalimbali ikiwemo katika chaguzi mbalimbali za Ubunge na Udiwani.


“Nimewaona kule Buhingwe nawapongeza sana hongereni sana mmefanya kazi nzuri nawapenda mlioshiriki Kibondo na kule Shinyanga hongereni sana tukaenda kushiriki Konde pia hapa karibuni pia tumeshiriki Ngorongoro na kote tumefanya vizuri,”amesema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post